Bukobawadau

NHC watoa miezi miwili kwa wadeni wake

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeipa notisi ya
miezi miwili Wizara na taasisi za serikali zinazodaiwa na shirika hilo wawe wamemaliza madeni yao kinyume na hapo watafunga ofisi kwa makufuli

Kati ya wizara zinazodaiwa na shirika hilo ni pamoja na JWTZ, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa linadaiwa billion 2, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Jeshi la Polisi, Mawasiliano na Uchukuzi pamoja na Wizara ya Ujenzi.

Bodi ya Usajili wa Waandisi, Wizara ya Kilimo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Utamaduni, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Maendeleo ya Vijana.

Nyingine ni Idara ya Habari Maelezo ambapo tayari wameshatolewa vifaa vyao vya kazi nje ya jingo hilo, Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, Tume ya Haki za Binadamu na Haki na Utawala Bora, Msajili wa Mahakama Kuu Tanga, Ofisi ya Rais, Tumre ya Utumishi wa Umma na Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Akizungumza na vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba (NHC), Bw. Nehemiah Mchechu alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya wadaiwa hao kuomba muda wa mwezi mmoja ili kulipa madeni yao.

Alisema tasisi hizo zimeomba shirika hilo muda huo ili kuweza kumaliza muda wao na wasiwatolee vyombo vyao nje kama inavyopanga shirika hilo.

Alisema endapo malimbikizo hayo hayatalipwa kwa kipindi hicho basi wataendelea na utaratibu wao huo wa kuzifunga ofisi hizo na kuwakabishi madadali kupiga mnada mali za wadeni hao ili kupata fedha zao wanazodai.

Alisema hatua hiyo pia imekuja kwa kuwa shirika hilo lina kazi kubwa ya ujenzi wa nyumba hivyo linahitaji fedha hizo ili kuweza kuanza ujenzi huo.

Pia alisema kuwa shirika hilo halina ugomvi na serikali bali wapo katika majukumu yao ya kikazi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau