Bukobawadau

SHUGHULI YA MAZISHI YA MAREHEMU OMLANGIRA JOHN MBONEKA HII LEO 1MARCH,2013 KIJIJINI BUGANDIKA

Camera yetu jioni hii imeweza kushiriki shughuli ya mazishi ya Marehemu John Luta Mboneko kijijini Bugandika,Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 90 ya kuishi,1923-2013.
Viongozi wa dini wakishiriki katika ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu John Luta Mboneko.
 Ibada ikiendelEA nyumbani kwa Marehemu Mlangira John Mboneko na kuudhuliwa na maelfu ya watu.
Mjane wa Marehemu John Mboneko, Bi Meria Nyakato Mtasa akiwa ni mke wa ndoa toka mwaka 1953 mpaka amebahatika kumpata mtoto mmoja wa kumzaa ambaye ni Bi Georgina.
Sehemu ya wachungaji wakishiriki ikibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Omlangira John Mboneko
Wachunguji na viongozi wa KKKT  Bukoba.
Mmoja wa wanaharakati wa kwanza kabisa nchini, Pichani kushoto habari juu yake itakua siku nyingine, leo hapa inahusu msiba tu!
Mdau Baba Felly katika shughuli ya Ibada.
Umati wa waombolezaji wakishiriki katika Ibada.
 Mdau Jamal Kalumuna akiwajibika.
 Mlangira Ben Kataluga katika pitapita za hapa na pale kuakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa.
Kapumzike kwa amani Marehemu John Mboneko.
 Hivi ndivyo ilivyo safari ya mwisho ya maisha ya Marehemu mzee wetu John Mboneko ,mcha mungu mwenye historia kubwa ya kimaisha ndani ya umri wake wa miaka 90 ya kuishi.
Mwili wa marehemu ukiingizwa kaburini.

Sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudi
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mhashamu Elisa Buberwao kutoka kwa Askofu Elisa Buberwa wa Jim akimkabidhi udongo Askofu mstaafu Mshemba.
 Askofu mstaafu Mshemba akiweka udongo kaburini.
Viongozi mbalimbali wa Kilutheri wameweza kushiriki mazishi haya.

Mdau Mama Elizabeth Lulu(katikati),katika uzuni mkubwa wa kuondokewa na Mzee wake mlezi.


Anaonekana Mlangira Daudi akisogelea mashada ya maua.
 Shada la ushirika wa Bukoba.
 Wananzengo kutoka jijini mwanza wakiweka mashada ya maua kaburini.
 Mlangira Focas Lutinwa akiweka shada lake kaburini.



Mwananzeng Ruge Mashanda wa Katabaro(home boy)pande hizi za bugandika.


Mrs Deo  Rugaibula na Mdau Divoth Rugaibula wakiwasili msibani hapa.

Mdau Thomas na Mdau Msafiri wakiwa eneo la tukio
Camera yetu ikiangaza pande mbalimbali.
 Sehemu ya waombolezaji katikat ni Mdau Mama Fready(Ma rihoba)
 Baada ya Shughuli ya mazishi , neno la shukrani kwa niaba ya familia likitolewa na Mtoto pekee wa kuzaliwa na Marehemu Mlangira John Mboneko , Bi Georgina,Juu ya alichokisema unaweza kupitia video yetu hapo juu au tembelea account yetu ya Youtube kwa kuandika neno Bukobawadau
Wachungaji katika utambulisho, kushoto ni Mchungaji Bugae Edwin wa Itawa, Mchungaji Rwegalula wa Kanyangeleko na Dini wa Nshombo.
Watu ni wengi kwelikweli.
 Kabla ya kuwarudisha wafiwa ndani Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mhashamu Elisa Buberwao akapewa nafasi ya kutoa neno.

BUKOBAWADAU BLOG Tunatoa pole kwa familia ya Marehemu  John Mboneko ikumbukwe
Kazi ya Mungu haina makosa na Binadamu hupanga wakati ... Lakini ni kazi ya Mungu hatuna jinsi zaidi ya kumuombea Maremu apumzike kwa amani!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau