Bukobawadau

KINANA AICHANACHANA CHADEMA MBEYA, AMALIZA ZIARA KWA KISHINDO

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda bajaji tayari kwa kuelekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe Mwanjelwa jijini Mbeya akitokea ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, huku Nape Nnauye naye akijiandaa kuinga kwenye bajaji. Kinana akiongozana na Ujumbe wake pamoja na viongozi wa mkoa wa Mbeya na wilaya leo wametumia usafiri huo ili kuonyesha kwamba Chama hicho ni chama cha wananchi wa kawaida ambao ni wafanyakazi na wakulima tofauti na wenzetu wanaojifanya wanawatetea lakini wanakuja na Helikopta na kuwachangisha michango ya fedha kisha wanatokomea zao. Katika msafara huo pia yupo Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa kuteuliwa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-
Vijana wa Mwanjelwa wakiuzuia msafara wa Kinana wakati alipokuwa akielekea uwanja wa Luanda Nzovwe kwenye mkutano jambo lililofanya Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye watembeee kwa mguu(P.T)
Next Post Previous Post
Bukobawadau