Bukobawadau

MDAU BYABATO ANAHOJI;Wana Kagera wa Dar misaada yenu inawafikia walengwa?

Sipendi kubeza jitahada za wadau hasa wanaoishi katika jiji la shida na raha la Dar salaam kuendesha harambee na harakati za kuchangia sekta kadha katika mikoa ya walikozaliwa.Matukio ya aina hii ni mengi lakini leo naongelea ‘harambee ya kuchangia maendeleo ya jimbo la Nkenge’ iliyofanyika jijijini Dar na kuhudhuria na makamu wa rais dk ghalib bilali ambapo jumla ya fedha sh milioni 114 zilichangwa na kati yake milioni 65 zikiwa ni taslimu.Nawapongeza waandaaji na waliochanga!.

Kwa kuwa tukio kama hili liliwahi kufanyika kwa jina la ‘Kagera day’ na taarifa ni kwamba mamilioni yaliyochangwa wakati huo yakilenga kuboresha elimu mkaoni humo yalitafunwa na ‘wajanja’ hadi kusababisha serikali ya mkoa kutoa ufafanuzi ‘mwepesi’ juu ya kufunjwa kwa hizo fedha.


Soma hapa…

TOVUTI YA MKOA WA KAGERA ...............

Sasa juzi wadau wamerudia makosa yale yale (kwa maoni yangu) kufanya harambee kama hiyo eti wanalenga kutatua tatizo la madawati katika wilaya ya missenyi.


Nimekuwa kizunguka katika shule za msingi na sekondari wilyani humo wala sijui nani alifanya utafiti wa kubaini kwamba suruhisho la kuboresha elimu wilayani humo ni kuchangisha fedha ili wanunue madawati.

Soma hapa 
DKT.BILAL AENDESHA ZOEZI LA HARAMBEE YA KUCHANGIA MADAWATI MFUKO WA MAENDELEO YA ELIMU JIMBO LA NKENGE - Kagera Yetu

1.Je hizo fedha zitawafikia walengwa? Kwa njia gani

2.Nkenge Foundation ni mali ya nani? Imesajiliwa kwa jina la nani? 
3.Nani msimamizi wa hizo fedha,ziko kwenye account ya nani?
4.Hizi hazitafunjwa kama zile za kagera day ?
5.Hakuna malengo ya kisiasa katika hizi harambee? Yasipotimia itakuwaje?

Ninaomba wenye michango ya kujenga kagera na taifa kwa ujumla tujadili kwa maslahi kuntu.


M.Byabato

Bukoba
cc. Phinias Bashaya Anna Tibaijuka @Ta Muganyizi
Next Post Previous Post
Bukobawadau