Bukobawadau

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAFUKUZA KAZI MAWAZIRI WANNE,SIKILIZA AUDIO YA WAZIRI MKUU AKITOA TAMKO BUNGENI

SIKILIZA AUDIO YA WAZILI MKUU AKITOA TAMKO BUNGENI HAPO JUU WAZIRI 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki ametangaza Bungeni kuwa amejiuzulu kutoka katika wadhifa wake huo kutokana na Ripoti ya Kamati iliyoundwa kuchunguza madhila yaliyotokana na Operesheni Tokomeza Ujangili, operesheni iliyotekelezwa na Wizara yake ikishirikiana wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). Kagasheki alitoa kauli yake hiyo na kusema kuwa anapaswa kuwajibika, mara tu alipozungumza baada ya Wabunge kuchangia hoja hiyo iliyotikisa Bunge na kuleta simanzi kubwa kutokana na unyama uliofanywa dhidi ya wananchi ikiwemo kuteswa, kubakwa kwa wanawake na wengine kuuawa, adha iliyoikumba pia mifugo. , Kagasheki alisema anapaswa kuwajibika. Taarifa zaidi za Bungeni zimesema kuwa Rais Kikwete amepokea ripoti husika na kuridhia kuwafuta nafasi za uwaziri mawaziri wanne. Uamuzi huo ambao umesomwa na Waziri Mkuu, Mizengo PInda umewataja mawaziri waliofutwa kazi kuwa ni Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vua Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Mathayo David Mathayo (MIfugo na Uvuvi) na Hamisi Kagasheki (Maliasili na Utalii).
Next Post Previous Post
Bukobawadau