Bukobawadau

UPDATES: LOWASSA ANUSURIKA KATIKA AJALI YA NDEGE JIJINI ARUSHA LEO

Habari zimetujia sasa hivi zinasema abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli  Mh Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuwa pasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Arusha leo mchana. 
Ndege hiyo ya shirika la ndege la precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua, ambapo Matairi yote manne ya nyuma yalipasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria.
"Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.
 Mh Lowassa ni mbunge wa Monduli, jimbo ambalo anatoka Waziri Mkuu aliyekuwa kipenzi Cha mwalimu Nyerere na watanzania hayati Edward Moringe Sokione.Sokoine aliyefariki katika ajali ya gari mwaka 1994.
 UPDATES KUTOKA ABIRIA MWINGINE:Nikiwa mmoja wa abiria tuliosafiri na PW kurudi Arusha leo, ndege ya shirika hilo yenye usajili No 5HPWI imepata kizaazaa wakati wa kutua baada ya tairi mojawapo kupasuka kwa kishindo, likufuatiwa na mengine yote ya nyuma ambapo yalipasuka pia na kuacha vipandevipande kwenye njia ya kurukia.

Waliookota vipande hivyo wamesema kuwa wamekuta viraka(pechi, watu wa magari wananielewa zaidi hapa), kitu ambacho si kawaida kwenye usafiri wa jamii hii!

Rubani wa ndege hiyo amejitahidi kuitoa ndege hiyo nje ya njia ili kutozuia ndege nyingine kuruka, japokuwa mwishowe ilimgomea kabisa na kubaki ikisota pembeni mwa njia hiyo.

Kikubwa ni kwamba hakuna madhara yaliyowapata abiria, akiwemo Bwana Lowassa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau