Bukobawadau

Upimaji ardhi Ngara waendelea

ZOEZI la upimaji ardhi na utoaji wa hati za kimila kwa wananchi wa Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera unaendelea ili kuandaa matumizi bora ya ardhi katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Constantine Kanyasu, alibainisha hayo alipokuwa akisoma taarifa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira katika ziara yake mkoani Kagera mwishoni mwa wiki na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya upimaji wa ardhi.
Alisema jumla ya vijiji 72 kati ya 68 vimeshapimwa na vimeshaandaliwa hati za kimila huku vinne vimeandaliwa mpango wa matumizi bora ya ardhi  ya kijiji.
Kanyasu alisema utaratibu huo uliofanywa na serikali wa kuanzisha  utaratibu wa kutambua mali za wanyonge utawasaidia ikiwa ni pamoja  na kutambua ardhi inayomilikiwa na wananchi  kwa hatimiliki za kimila.
Alieleza uandaaji wa hatimiliki za kimila unaendelea na hadi sasa jumla ya hati 1,000 zimeshaandaliwa, hati 800 zimechapwa na 710 zimeshagawiwa kwa waombaji mbalimbali kwenye vijiji husika.
Next Post Previous Post
Bukobawadau