Bukobawadau

HUKO MBEYA WAPORA MAITI BAADA YA KUCHOSHWA NA IBADA

Picha hii tulikutana nayo mwisho mwa 2011, Maiti ya Mama ikiwa na Mtoto Tumboni, Mama HUYO ALIKUFA baada ya kushindwa kujifungua ,Hapa ni maeneo ya Rutenge, Maiti ikisafirishwa kutoka hospital ya Ndolage Kamachumu kuelekea kijijini Ichwandimi/Rubale umbali wa KM 80 hivi.(Bukobawadau Blog tunatumia fursa hii kuwaombea na kuwakumbuka wazazi wetu/walezi waliopoteza maisha wakati wa kujifungua.Amen!!


Mbeya. Kundi la vijana 60, juzi walipora mwili wa marehemu Gabriel Ngalele ukiwa unaombewa kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG) eneo la Uyole jijini baada ya kuchoshwa na ibada ndefu ya mchungaji.
Ibada hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Mchungaji, Edward Mtweve wa kanisa hilo ambaye alijikuta kwenye mazingira magumu baada ya vijana hao wanaodaiwa kuwa ni madereva wa pikipiki kuvamia madhabahu na kubeba sanduku lililokuwa na mwili wa marehemu.
Marehemu Ngatele alikuwa dereva wa pikipiki na alifariki kwenye ajali iliyotokea eneo la Sae baada ya pikipiki yake kuligonga lori lililoharibika katikati ya barabara. Katika ajali hiyo, abiria pia alifariki.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika kanisa hilo, na wakati mchungaji akiendesha ibada kulijitokeza kelele za hapa na pale na kusababisha mchungaji kuomba utulivu mara kadhaa.
Lakini kelele nyingi zililipuka ghafla zikiwamo za kulalamika kwamba ibada ilikuwa ndefu na hatimaye vijana wengi walionekana wakiingia kwenye mlango na kuvamia madhabahu na kutoka na mwili wa marehemu.
Baada ya kuuchukua mwili, vijana hao walikwenda kwenye makaburi kuuzika wakati naye mchungaji akiendelea kuhubiri waumini waliobaki ndani ya kanisa.
Mchungaji Mtweve alilazimika kwenda nyumbani baada ya kumaliza ibada badala ya makaburini, huku vijana nao wakiendelea na taratibu za mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa waendesha pikipiki Mbeya, Vicent Mwashoma.
Mwendesha pikipiki aliyetajwa kwa jina la Bahati Mwasote alilazimika kuendesha ibada ya mazishi.
Mchungaji Edward Mtweve alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema alisikitishwa na kitendo cha kuvurugwa kwa ibada.
Next Post Previous Post
Bukobawadau