Bukobawadau

JAHAZI WAFAFANUA KUTAMBULISHA NYIMBO MPYA MOROGORO

KUNDI la Jahazi Modern Taarab limefafanua ni kwa nini limeamua kuuchagua mji wa Morogoro kama kituo chao cha kwanza cha kutambulishia nyimbo zao mpya zitakazounda albam yao mpya ijayo.Jahazi wanatagemewa kufanya onyesho maalum Morogoro kwa ajili ya kuwaonyesha nyimbo mpya mashabiki wao Ijumaa ya tarehe 31 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Tanzanite Complex.
Kiongozi wa Jahazi Modern Taraab, Mohamed Mauji, jana alifanya mahojiano na kipindi cha Sham Sham za Pwani cha ITV kinachoongozwa na mtangazaji Hawa Hassan (kama wanavyoonekana pichani) ambapo msanii huyo alitoa sababu kadhaa ni kwanini wameichagua Morogoro. Kipindi hicho kitaruka hewani tena Jumamosi hii saa 11 jioni.
Mauji ambaye ni mcharazaji gitaa la solo, alisema  miongoni mwa sababu nyingi  ni pamoja na kuwa mji wa Morogoro ni ngome yao kubwa (ukiondoa Dar es Salaam)  hivyo safari hii wameupa heshima ya kipekee.
Mara zote Jahazi imekuwa ikianza kutambulisha nyimbo mpya jijini Dar es Salaam na baadaye kufuatiwa na uzinduzi na baada ya hapo ndipo wanazipeleka nyimbo mpya mikoani.
Mauji pia katika mahojiano yake hayo alifichua mikakati yao mikubwa ya kukakabiliana na ushindani kwa mwaka huu wa 2014.
Next Post Previous Post
Bukobawadau