Bukobawadau

TASWIRA MKUTANO WA CHADEMA OPERESHENI PAMOJA DAIMA MJINI BUKOBA LEO JAN 26,2014

Mwanzo wa harakati za M4C -PAMOJA DAIMA ndani ya Manispaa ya Mji wa Bukoba leo ambapo Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) kinaendelea kupasua anga kwa kutumia Helkopita ili kuwafikia wafuasi wao kwa haraka
Chopa ya Chadema ikiwa katika viwanja vya Uhuru mjini hapa
 Muda mfupi baada ya helikopta kutua katika viwanja vya uhuru Mjini Bukoba
Hekaheka baada ya helikopta kutua
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwasili katika viwanja vya Uhuru Platform mjini Bukoba kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika  leo Jan 26,2014
 Wakazi wa mji wa Bukoba na vitongoji vyake wakiwa pembezoni mwa viwanja vya uhuru
 Anaonekana Mh. Richard katikati, Diwani CCM miembeni

 Picha mbalimbali za Matukio ya mkutano wa hadhara wa chadema Operesheni M4C Pamoja Daima,uliofanyika kwenye Uwanja wa uhuru Uswahilini  jioni ya leo
Baadhi ya wananchi wa mji wa Bukoba wakiwa wametulia wakati wa mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima wa Chadema, uliofanyika kwenye Uwanja wa uhuru
Hotuba zote Audio na video zinapatikana hapa hapa bukoba wadau blog.Ukianzia mwanzo wa habari iliyopo juu ya hii, Picha zaidi zinapatika kwenye ukurasa wetu wa facebook.
Mwenyekitiwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe  akihutubia mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye uwanja wa uhuru  leo.
 Wakiitikia kwa pamoja  'peoplespower'.
 Kama kawaia Mh . Mbowe akiendelea kufanya makamuzi
Sehemu ya wanahabari wakisikiliza hotuba ya Mbowe .
 Mwenyekitiwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe akiendelea kuhutubia mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima
 Mdau akikomaa na matukio mwanzo mwisho

Makamu Mwenyekiti wa chadema  Zanzibar, Mh.Said I. Mohamed akiwahutubia wakazi wa Bukoba
 Wadau na nyuso za furaha  
Makamu Mwenyekiti wa chadema  Zanzibar, Mh.Said Issa Mohamed akiendelea kuhutubia katika mkutano wa Operesheni Pamoja Daima Mjini Bukoba.
 Godbless Jonathani Lema Mbunge Jimbo la Arusha mjini(Chadema) akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Bukoba na Vitongoji vyake leo Jan 26, 2014
Wananchi wakiendelea kumsikiliza Mh. Lema.
 Wafuasi wa CHADEMA wakimsikiliza Mbunge Jimbo la Arusha mjini(Chadema ) Godbless Lema alipokuwa akiwahutubia leo katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima
Mbunge Concesta Rwamlaza Chadema viti Maalum (Bukoba) azungumza juu ya hali mgogoro wa kisiasa ndani ya Manispaa ya Mji wa Bukoba
 Matukio zaidi yanapatika kupitia ukurasa wetu wa facebook
 Wanaume kazini.
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare akiwahutubia maelfu ya wananchi  mjini Bukoba katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima uliofanyika leo Jan 26,2014 katika uwanja wa Uhuru( Mayunga)

 Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatarekatika hali ya usikivu.
Sehemu ya wanahabari wakiwajibika.
Mkutano ukiendelea wakazi wa Manispaa ya Mji wa Bukoba wakimsikiliza Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika
Mh.Mbunge wa Ubungo John Mnyika akiwahutubia wananchi wa mji wa Bukoba na vitingoji vyake katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima
  Mbunge wa Biharamulo Magharibi Dk.Anthony Mbassa akiwahutubia wananchi wa mji wa Bukoba na vitingoji vyake katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima
Sehemu ya Mamia ya wakazi wa Manispaa ya Bukoba  waliojitokeza katika mkutano wa Operesheni Pamoja Daima ulio ongozwa na  Mh Freeman Mbowe
 Mamia ya wakazi wa Manispaa ya Bukoba  waliojitokeza katika mkutano wa Operesheni Pamoja Daima ulio ongozwa na  Mh Freeman Mbowe,Mh Lema, Mh. John Mnyika na Dk.Anthony Mbassa na Makamu Mwenyekiti wa chadema  Zanzibar, Mh.Said Issa Mohamed
 Mwisho wananchi wakiwa wamesimama tayari kwa kidedea kuwasindikiza Viongozi wa Chadema
 Mwanzo wa Msafara wa maandamano baada ya Mkutano kufungwa.
 Viongozi wa Chadema wakiondoka kwa shamrashamra, baada ya kuhutubia mkutano wa hadahara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika katika mjini Bukoba leo.
 Mashamsham,Ngembe na vikeleshendo wafuasi wa Chadema wakitoa  sopport ya aina yake
Wafuasi wa Chadema katika kidedea kuwasindikiza Viongozi wa Chama chao.
 Kidedea katikati ya Barabara ya Jamhuri.
Kutoka uwanja wa Uhurus moja moja hadi stand kuu ya mabus,kukatiza barabara ya tupendane mpaka Jamhuri na sasa  makanda ndio haooo..wanaitafuta Uganda road hadi mwisho Victorious  Perch Hotel walipofikia Viongozi wa Chadema.







Next Post Previous Post
Bukobawadau