Bukobawadau

GLOBAL BREAKING, TAMASHA LA JOGGING WAAHIDI MAKUBWA DAR LIVE J’PILI HII

Kutoka kushoto ni mratibu mwenza wa Tamasha la Jogging, Mashauri, Mratibu wa Jogging, KP, Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, Mratibu wa Matukio wa Global, Luqman Maloto na Meneja wa Stamina, Said Ramadhani 'Kabwela'.
Abdallah Mrisho akisisitiza jambo katika mkutano huo na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Mkutano ukiendelea.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Mwanamuziki wa Bendi ya Msoondo Ngoma, Said Mabela akizungumzia maandalizi yao katika bonanza hilo.
Mambo yameiva! Waratibu wa lile tamasha kubwa la mbio za taratibu (jogging) na huduma ya habari mpya zilizotokea punde ya Global Breaking News chini ya Global Publishers wameahidi kufanya makubwa ndani ya Dar Live Jumapili hii.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza ya Afrika-Sana, Dar leo asubuhi, meneja mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ alisema kuwa shughuli itakuwa nzito hivyo watu wafurike kwa wingi kushuhudia burudani ya aina yake.
“Baada ya jogging, kutakuwa na burudani kubwa ya muziki kutoka kwa wasanii wakubwa, Nay wa Mitego, Stamina, H. Baba na bendi inayopendwa na wengi ya Msondo,” alisema Abby Cool huku akisisitiza kuwa kwa mara ya kwanza Dar Live itaangusha burudani ya nguvu bila kiingilio.
Kwa upande wake, mratibu wa tamasha hilo la jogging, KP amesema: “Jogging itaanzia pale Uwanja wa
Taifa hadi Dar Live. Vikundi zaidi ya 150 vimethibitisha kushiriki. Watu waje kwa wingi kuona mambo matamu bure kabisa kwani hakutakuwa na kiingilio.”
Naye meneja wa msanii Stamina, Kabwela aliahidi kuwa Stamina amejipanga kufunika vibaya siku hiyo kwani amekuwa kwenye mazoezi ya kufa mtu.
Mbali na Jogging, Breaking News, pia Global Publishers imetambulisha shindano lake jipya la Global Star Search litakaloanza hivi karibuni kwa lengo la kuibua vipaji na kutengeneza ajira kwa vijana.
PICHA HABARI NA ERICK EVARIST/GPL
Next Post Previous Post
Bukobawadau