Bukobawadau

UAMUZI WA MUSEVENI WAITIA KIWEWE MAREKANI

Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Kampala. Siku moja baada ya Rais Yoweri Museveni kusaini sheria inayotoa adhabu kali kwa wapenzi wa jinsi moja, Marekani imesema inaangalia upya uhusiano wake na nchi hiyo kama ilivyoainisha awali
Katika taarifa yake iliyotolewa jijini Washington DC jana, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry alisema Serikali ya Rais Barack Obama itahakikisha ushirikiano wowote na Uganda utachujwa kupitia sheria za kupinga ubaguzi ambazo inazisimamia.

"Sheria imeshapitishwa, tunaanza kuchuja uhusiano wetu na Uganda kwa kuangalia mambo muhimu, ikiwemo maeneo tunayowawezesha," alisema Kerry katika taarifa yake jana.

Awali, akitia saini muswada huo kuwa sheria juzi, Rais Museveni alipuuza vitisho vya Marekani na kusema mataifa ya nje ambayo yamekuwa yakimtaka asisaini muswada huo pamoja na viongozi wa kidini hawana nafasi katika mambo ya ndani ya nchi yake.
"Watu kutoka nje hawawezi kutuamuru tufanye au tusifanye mambo yetu. Kama hawataki kwenda nasi, basi wanaweza kuchukua misaada yao," alisema.

Pia, inatoa kifungo cha hadi miaka 10 kwa kuonekana hadharani wakijiachia kama wapenzi.

Katika eneo la Kaskazini linalotawaliwa chini ya sheria za Kiislamu, wapenzi hao wanakabiliwa na adhabu ya kifo.

Cameroon ni miongoni mwa nchi zenye sheria za aina hiyo, ambapo wapenzi wa jinsi moja wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka mitano jela.

Gambia imekuwa na mfumo wa sheria dhidi ya wapenzi wa jinsi moja wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 14 jela na kazi ngumu.

Nchini Zambia pia, wapenzi wa jinsi moja walipigwa marufuku tangu enzi za utawala wa Waingereza na waliobainika, walikabiliwa na kifungo cha hadi miaka 14 jela.

Kwa upande wa Senegal, yeyote atakayetiwa hatiani kwa kujihusisha na kitendo chochote kisichokuwa cha asili na mtu wa jinsi yake anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela.

Nchini Tunisia, vitendo vya uhusiano ya wapenzi wa jinsi moja kwa watu wazima hukabiliwa na adhabu ya hadi miaka mitatu jela.

Nako Morocco, wenye tabia hiyo hukabiliwa na kifungo cha kuanzia miezi sita hadi miaka mitatu jela.

Kule Algeria, yeyote anayetiwa hatiani kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja anakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela, lakini wengi huweza kushikiliwa kwa muda usiojulikana.

Nchini Zimbabwe, Rais Robert Mugabe amekuwa akisisitiza kwamba wapenzi wa jinsi moja ni wabaya kuliko nguruwe na mbwa.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba makundi ya watu wa aina hiyo yanaruhusiwa katika baadhi ya maeneo.

Nako Malawi, Novemba mwaka 2012, Rais Joyce Banda alizuia sheria za kupiga marufuku wapenzi wa jinsi moja hadi zitakapojadiliwa bungeni. Kwa sheria iliyopo, wanaume wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 14 jela na wanawake hadi miaka mitano jela.
Nchi nyingine zikiwamo Chad, Gabon, Ivory Coast na Mali hazijapiga marufuku, lakini Afrika Kusini iliruhusu ndoa za jinsi moja mwaka 2006.

Pamoja na hatua hiyo, wapenzi wa jinsi moja wamekuwa wakidhibitiwa ipasavyo kwa kuadhibiwa iwe wanaume au wanawake ili kuwarejesha kwenye mfumo wa kawaida.

Wapenzi wa jinsi moja waanikwa

Jarida moja nchini Uganda limechapisha orodha ya majina na watu 200 liliowataja kuwa wapenzi wa jinsia moja, siku moja baada ya Rais Yoweri Museveni kutia saini sheria inayowabana watu wa namna hiyo.

Jarida hilo lililopewa jina la Red Pepper lilichapisha majina hayo jana pamoja na picha za wahusika katika ukurasa wake wa mbele, chini ya kichwa cha habari: "WAANIKWA!"

Orodha hiyo inajumuisha wanaharakati maarufu wa haki za mashoga wa Uganda, akiwemo Pepe Julian Onziema ambaye mara kadhaa alionya kwamba sheria hiyo ya kuwabana wapenzi wa jinsi moja itaibua machafuko. Msemaji wa Polisi wa Uganda, Patrick Onyango alisema hata hivyo hakuna wahusika waliokamatwa tangu Rais Museveni alipotia saini sheria hiyo juzi, lakini tayari hakuna msalie mtume kwa wale watakaotiwa nguvuni.

Msimamo wa Museveni

Akitia saini muswada huo kwenye Ikulu ya Eenrebbe mbele ya wanahabari na maofisa wa juu wa Serikali yake juzi, Museveni mbele ya maofiosa wa juu wa Serikali yake na waandishi wa habari, alisema adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wale watakaopatikana na hatia kwa mara ya kwanza haiepukiki. Pia, adhabu ya maisha jela itatolewa kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja zaidi ya mara moja kati ya watu wawili waliokubaliana kufanya hivyo.

Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi

Akizungumzia onyo lililotolewa na baadhi ya viongozi wa kidini akiwemo Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini, Museveni alisema: "Kumbuka hata Yesu aliuawa na maaskofu, ndiyo maana huwa sisikilizi watu hao (viongozi wa kidini)."

Mataifa ya Afrika yenye sheria kama iliyopitishwa Uganda

Wakati Marekani na baadhi ya washirika wao wakitishia kuzuia misaada kwa Uganda, mataifa mengi ya Afrika, isipokuwa Afrika Kusini yana sheria kali za kupiga marufuku wapenzi wa jinsi moja. Sheria zimekuwa zikitekelezwa kwa muda mrefu sasa.

Shirika la Haki za Binadamu, Amnesty International linasema uhusiano wa kimapenzi wa watu wa jinsi moja umeharamishwa kisheria katika nchi 38 kati ya 54 barani humo na adhabu ya kifo imehalalishwa nchini Mauritania, Sudan na Somalia.

Nchi zilizoweka sheria kali kuwabana wapenzi wa jinsi moja ni pamoja na Uganda ambayo imepiga marufuku wapenzi wa jinsi moja na kutoa adhabu ya hadi kifungo cha maisha gerezani kwa wale wanaorudia vitendo hivyo.(E.L)
Sheria hiyo inazuia kutangaza masuala yahusuyo wapenzi wa jinsi moja na kuwataka watu kuwatenga na kuwakataa mashoga.

Nigeria, pia imeweka sheria maalumu iliyoanza kutekelezwa Januari mwaka huu. Sheria hiyo inatoa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 14 jela kwa wapenzi wa jinsi moja wanaoishi pamoja.
Next Post Previous Post
Bukobawadau