Bukobawadau

WATAKIWA KUANDIKA NA KUTANGAZA HABARI ZA UCHUNGUZI

Wanahabari wa kituo cha radio kwizera katika wilaya ya ngara mkoani kagera wametakiwa kuandika na kutangaza habari za uchunguzi ili kuondoa ama kupunguza changamoto mbalimbali zilizoko kwenye jamii
Wito huo umetolewa kwa wanabari wa kituo hicho walipokuwa katika mafunzo ya siku sita  kujiongezea uwezo katika taluma yao ili kuweza kuboresha utendaji kazi katika majukumu ya kila siku.
Wanahabari hao wameaswa kutojiona wao ni wenye ujuzi katika kutafuta na kuandika habari kisha kuonekana wenye kutoa hukumu bali wazingatie miiko ya taaluma ya habari na kulinda maadili ya kazi yao

Mafunzo hayo yalilenga kuandik habari za uchunguzi kutoka kwenye jamii inakosikika radio kwizera  katika baadhi ya wilaya ya za  mkoani kagera na wilaya zote zilizoko mkoani kigoma

Mafunzo hayo yaliendeshwa na mkufunzi mwanahabari mkongwe hapa nchini Bw Philli karashani ambaye aliwaasa wanabari hao kufanya kazi wakijikinga na maisha yao katika mazingira ya habari za uchunguzi

Karashani alisema baadhi ya habari zina hatari  ya kupoteza maisha na wasijirahisi kwa kujenga mahusiano ya karibu na vyanzo vya habari kwani baadhi yake vinaweza kuw chanzo cha kuhatarisha maisha ya kiutendaji

"Kuandika na kutangaza habari za uchunguzi  ni pamoja na kuibua changamoto zilizoko kwenye jamii hasa katika sekta ya afya maji elimu Biashara  migogoro ya ardhi".Alisema Karashani

Aidha Afisa uzalishaji wa vipindi vya radio kwizera Bi Joyce Ngalawa aliwasisitiza wanahabari wenzake kuhakikisha habari zinazoandikwa zinakuwa za kuelimisha na kuondoka kero za kijamii pasipo kutengeneza makundi ya kuhatarisha usalama na amani
"Jambo la kujivua katika kuandika habari ni pale habari zitakapo andikwa na kutangazwa kisha kuleta manufaa kwa wananchi ama jamii iliyokusudiwa".Alisema Bi Ngalawa

Pamoja na hayo  mkurugenzi wa kituo hicho Fr Damasi Misanga alisema baadhi ya wanahabari walioko katika vituo vya mbali kama biharamulo kibondo kasulu kakongo na maeneo mengineyo
(Reporters) watapatiwa vitendea kazi hasa simu zenye kuunganishwa na  mitandao ya mawasiliano ili kurahisisha utendaji kazi bora na kufikisha habari kwa haraka.

Na Shaaban Ndyamukama
Next Post Previous Post
Bukobawadau