Bukobawadau

CHECK HAPA CHATU ALIVYO MDHIBITI MAMBA NA KUMLA

Anaonekana Nyoka aina ya Chatu alijipinda kwa Mamba na kumbana hadi akafa
 Mamba hoi akitolewa ndani ya Maji 
 Chatu huyo alianza kumla Mamba na kushangaza wakazi
 Baada ya mlo huo mkubwa Nyoka akichukua zake kesi
Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla.
Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.
Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.
Tiffany Corlis,mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi.
"lilikuwa jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC.
"Tulimuona Nyoka akipambana na Mamba, alifanikiwa kumpinda mamba na kumzunguka hasa katika sehemu ya miguu yake ili kumdhibiti.''
"pambano lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''
"Baada ya Mamba kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kunza kumla,'' alisema Tifanny.
Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua Nyoka dakika kumi na tano kuma yule Mamba.
''Bila shaka Nyoka huyo alishiba vyema, na hatuui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.
Mtu mwingine aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili walipambana kwa karibu masaa 5. Hatimaye wote walionekana kuchoka.
''Sio kitu unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce.
BBCSwahili
Tupo naITEMBWE GENERAL SUPPLIES wasambazaji wa ving'amuzi vya Star Times Mjini Bukoba,Star Times wana lengo la kuifanya kila familia ya Afrika iweze kununua, kutazama, na kufurahia zaidi matangazo ya televisheni ya digital kwa muda na wakati sahii
Kampuni ya StarTimes inakubalika na nembo yake inajulikana na kila familia na kwa kila mtu!!!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau