Bukobawadau

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWA UFUPI UZINDUZI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA MARCHI 21,2014


- Wajumbe mhakikishe mnatunga Katiba itakayodumisha Muungano wetu
- Tunahitaji Katiba itakayodumisha Amani na Usalama wa nchi yetu!
- Ni mara ya TATU kwa Tanzania kuwa na mchakato wa kutunga Katiba Mpya! 1965, 1977 na sasa 2014!
- Tofauti na awamu zilizopita za michakato ya kutunga Katiba, awamu hii imewahusisha wananchi kwa ukaribu zaidi!
- Mchakato wa sasa utaishia kwenye Kura ya Maoni ili wananchi wachukue maamuzi wenyewe!
- Katiba ya sasa ya Tanzania imefanyiwa mabadiliko kwa takribani mara 14 tokea mwaka 1967!
- Serikali imekuwa tayari kufanya mabadiliko ya Katiba kila ilipoonekana kuwepo uhitaji wa kufanya hivyo!
- Wapo watu walioifananisha Katiba yetu na nguo yenye viraka vingiiiii
- Wapo waliodai kuwa 'Tukipata Katiba Mpya tutaiondoa CCM Madarakani'
- Madai ya Katiba Mpya yaliibuka baada ya kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi Tanzania
- Mwaka 2010 mwezi Disemba nilisema 'Tutazindua Mchakato wa kupata Katiba Mpya'
- Mchakato wa Katiba Mpya utahitimishwa kwa wananchi kupiga Kura ya Maoni ili kuikubali au kuikataa Katiba Mpya!
- Kitendo cha Warioba kuwasilisha Rasimu mbele ya Bunge kinahitimisha rasmi kazi ya Tume. Kazi inayofuatia ni ya Bunge!
- Niliwaagiza Tume kuiweka Rasimu ya Katiba Mpya kwenye Tovuti ili wananchi waweze kusoma na kutoa maoni yao!
- Nawapongeza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kazi nzuri waliyoifanya. Haikuwa kazi rahisi
- Tume ya Mabadiliko ya Katiba imepokea maoni 772,211 toka kwa wananchi na kuyafanyia uchambuzi wa kina!
- Tume imefanya kazi nzuri, yenye manufaa kwa watanzania. Rasimu imeandikwa vizuri na mapendekezo yanayofaa!
- Rasimu ya Katiba ni kitabu chenye kurasa 106, sura 17 & Ibara 271. Wajumbe wa Bunge msome na kuelewa kila kilichoandikwa!
- Ni vema wajumbe wafanye uamuzi wenyewe sio wa kuambiwa na wenzao! [Akiwataka wasipelekeshwe]
- Wajumbe mjiridhishe na vifungu vyote kama vimeandikwa sawa; dhana zilizomo kwenye rasimu. Ni dhamana mliyopewa
- Tunachotaka watanzania ni KATIBA BORA! Msipofanya hivyo, kuna hatari ya kupata Katiba isiyotekelezeka!
- Bunge Maalum la Katiba lina wajibu wa kuliepusha Taifa na ulazima wa kufanya mabadiliko ya Katiba baada ya kutungwa!
- Yapo mambo mengi kwenye Rasimu Katiba ambayo yanahitaji wajumbe kueleweshwa ili waweze kufanya maamuzi sahihi
- Huwezi kudai PEPO ambayo huna uwezo nayo! Lakini kujipa matumaini ya Pepo ambayo huna uwezo nayo ndio uungwana...
- Ibara ya Pili ya Rasimu ya Katiba inayohusu MIPAKA ya nchi ina maelezo mazuri lakini haijagusia MAZIWA na MITO!
- Kama asemavyo Mtikila "Wakati wenyewe ndio huu!" (akiongelea mipaka ya nchi kuhusisha maziwa na mito)
- Mfumo wa Serikali 3 unaopendekezwa na Tume; mambo yanayohusu uchumi yapo chini ya mamlaka ya serikali za nchi husika!
- Suala la Kilimo na Pembejeo katika Rasimu ya Katiba kuachwa bila kutolewa ufafanuzi kwny Serikali 3 yataleta migongano
- Akili za kuambiwa, changanya na za kwako! ‪#‎KatibaMpya‬
- Kama wajumbe mkiamua kuendelea na serikali mbili, bado mambo yaliyopendekezwa na Tume yanatekelezeka bila tabu!
- Katika uandishi wa Rasimu, orodha ya Mambo ya Muungano suala la Utumishi halikuelezwa kama suala la Muungano!
- Katika Rasimu hii kuna mambo mapya ambayo yanabadili namna ya uendeshaji wa Serikali. Wajumbe muangalie kama yanafaa
- Ibara ya 128, ibara ndogo ya pili D. "Mbunge kuweza kupoteza ubunge endapo atashindwa kufanya kazi ya ubunge kwa miezi 6" iangaliwe
- Mbunge kuugua miezi 6 mfululizo na akapoteza nafasi yake ni kama ukatili wa hali ya juu!
- Itumiwe hekima kuviangalia vifungu kadhaa vyenye kuwa na matatizo na vinavyoweza kupelekea usumbufu usio na sababu
- Dhana ya Ukomo wa vipindi vitatu kwa Ubunge (tena bila kusema ni kwa mfululizo) nayo inahitaji kuangaliwa vema.
- Ni vema kuwa na ukomo kwa urais (akisema mtu anaweza kuigeuza nchi shamba), lakini ukomo kwa wabunge uangaliwe vema
- Dhana ya kwamba mbunge aliyepoteza nafasi yake chama chake ndicho kijaze nafasi yake iangaliwe kwa umakini isilete misuguano!
- Dhana ya Mawaziri kutokuwa wabunge ni nzuri lakini inahitaji kuangaliwa kwa umakini!
- Suala lililovuta hisia za watanzania wengi ni suala la Muungano wa Tanzania. Serikali 2 au Serikali 3!
- Nawaomba wajumbe mnapojadili aina ya Muungano unaofaa Tanzania muwe watulivu! Epukeni jazba!
- Madai ya Serikali Tatu si jambo jipya! Mwaka 1984 ilikuwa hoja iliyopelekea machafuko huko Zanzibar.
- Suala la Serikali Tatu Wajumbe mlizungumze limalizike. Kama zinakubaliwa, zikubaliwe; kama kukataliwa ijulikane!
- Kuna rai zinatolewa kuwa kwenye mjadala wa aina ya Muungano yasitumiwe majina ya Nyerere/Karume! Nadhani si sahihi
- Tume imedai Muundo wa Serikali 3 ndiyo matakwa ya watanzania walio wengi na imetoa sababu zake!
- Wapo wanaodai kuwa Takwimu za Tume yenyewe hazionyeshi ukweli kuwa watanzania wengi wanataka muungano wa serikali tatu!
- Inadaiwa kuwa 86.4% ya watanzania waliohojiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba hawakuwa na tatizo na muundo wa Muungano!
- Inadaiwa katika maoni yote ya Tume, ni 10.4% iliyoongelea muundo wa Muungano!
- Kuhusu usahihi wa hoja za wanaoikosoa Tume ya Mabadiliko ya Katiba juu ya aina ya Muungano, nawaachia wajumbe!
- Wapo wanaolalamika kuwa Zanzibar ina bendera yake, Katiba yake, Wimbo wake n,k
- Nimeeleza niliyoeleza kwa muhtasari; ninyi wajumbe ndio mna maamuzi juu ya aina ya muundo wa Serikali unaotufaa!
- Kuhusu muundo wa Serikali Tatu, Jaji Warioba alitutoa hofu kuwa "Gharama si kubwa sana za kutisha!"
- Wajumbe mjipe nafasi ya kulitafakari kwa undani suala la aina ya Muundo wa Muungano wa ‪#‎Tanzania‬
- Katika kujadili kwenu wajumbe, mtafute majibu muafaka ya matatizo yanayoweza kutokana na Muundo wa serikali tatu!
- Muundo wa Serikali tatu hautapunguza matatizo bali utaongeza matatizo kuliko ya sasa!
- Wapo wanaotaka Tanzania iingie OIC, wakisema kama Bara haitaki basi Zanzibar iachwe iingie...
- Wapo wanaotaka Zanzibar ijiunge na Umoja wa visiwa vya Bahari ya Hindi ili wanufaike huko, lakini wanaona wanabaniwa!
- Serikali zetu mbili zikiamua kuwa zinataka kutatua kero kubwa tatu za Muungano zilizobakia, zinatatulika!
- Kuna Mtanzania alitumia SMS akidai nimekula njama na Warioba na tunawatumia wapinzani kujiongezea muda hadi 2018!
- Serikali zetu mbili hazina kigugumizi cha kupunguza kero zinazoweza kupunguzika. Hakuna mwenye hila wala dhamira mbaya!
- Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964; mambo 11 ndiyo yalikuwa ya Muungano (kayataja)!
- Mwaka 1968 suala la mafuta, petroli na gesi asilia liliwekwa rasmi kwenye masuala ya muungano!
- Mwaka 1973 Baraza la Mitihani la Taifa liliingizwa kwenye orodha ya mambo ya Muungano
- Mwaka 1992 tulikubaliana kuwa Vyama vya Siasa viwe vya kitaifa, suala hilo likaingizwa kwny Orodha ya Mambo ya Muungano
- Tulikubaliana (Kikwete na Karume Jr) kuwa suala la Mafuta na Gesi asilia liondolewe kwenye mambo ya Muungano...
- Sisi kama CCM tunaweza kufanya mabadiliko muhimu katika Muungano bila kuhitaji serikali ya tatu!
- Mkitaka serikali tatu, ni lazima mtengeneze mazingira! Serikali ya Tatu ijulikane chanzo cha mapato yake.
- Hapa tunatengeneza nchi yetu, tutengeneze kitu kilicho thabiti!
- Serikali ya Muungano (katika serikali 3) inategemea majeshi ya Tanganyika na yale ya Zanzibar!
- Endapo majeshi ya Tanganyika na ya Zanzibar yakiigomea Serikali ya Muungano utekelezaji wa shughuli utakuwaje?
- Serikali ya tatu (ya Muungano) ni vigumu kukopesheka! Labda idhaminiwe na Tanganyika...
- Hata wanaopenda serikali tatu natambua wanapenda serikali iwe na nguvu. Lazima tujue changamoto zitakabiliwaje!
- Ningependa kama mnaamua tuwe na serikali tatu, basi ziwe tatu zinazosimama na thabiti!
- Watanzania zaidi ya 90% wamezaliwa baada ya 1964!
- Ikishatengenezwa Tanganyika, masharti yataibuka! Watu wataanza kuwa wageni... Watakaotoka upande wa pili wa Muungano
- Ikishazaliwa Tanganyika, chuki za Utaifa zinaweza kuanza; na zitatufikisha pabaya!
- Hata Tume ya Mabadiliko hawana majawabu ya uhakika juu ya kero zitakazotokana na serikali tatu!
- Kama mnaamua tuuvunje Muungano, vunjeni lakini si wakati nikiwepo!
- Kuna kiongozi mmoja wa dini aliniuliza, "Serikali 2 zikiwa na matatizo, dawa ni kuongeza ya 3?"
- Kazi iliyo mbele yenu wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ni nzito. Hatma ya nchi yetu ipo mikononi mwenu!
- Pandu Kificho akiwa Mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalum la Katiba alifanya kazi kubwa na nzuri!
- Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba walitumia muda mrefu kwa hatua ya kwanza, ni vema wajitahidi kuongeza kasi sasa!
- Hatua ya awali ya Bunge Maalum la Katiba iliwakwaza wananchi; natumaini kuanzia sasa hayatarudia yale yaliyotokea!
- Nawaomba wajumbe wote kauli mbiu iwe ‪#‎TanzaniaKwanza‬! Misimamo inayobomoa, ikiwa ya vyama au vikundi haina maana...
- Kura za NDIYOOO au SIYOOO hazitakuwa na nafasi; zipigwe kura. Ziwe za siri au wazi, hilo nawaachia!
- Katiba Mpya inaewezekana! Timiza wajibu wako...! Mungu ibariki
Next Post Previous Post
Bukobawadau