Bukobawadau

MAANDALIZI YA YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA MEI 2, 2014 MKOANI KAGERA

Mkoa wa Kagera uanendelea na Maandalizi ya uzinduzi wa Mbioa za Mwenge wa Uhuru Kitaifa utakaozinduliwa  Kaitaba Manispaa ya Bukoba tarehe 02/05/2014 kuanzaia saa moja asubuhi.
Katika maandalizi hayo shughuli mbalimbali za maandalizi zinaendelea mkoani hapa ambapo maandalizi ya uwanja wa kaitaba kuwekwa sawa yanaendelea, ujenzi na ukarabati wa mambo mbalimbali unaendelea kufanyika katika uwanja huo.
Kamati ya sherehe ya mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe inaendelea na vikao vyake  vya kufanikisha uzinduzi huo  ambapo kikao kimefanyika trehe  27/03/2014 aidha,  kikao kingingine kinatarajiwa kufanyika  15 April, 2014
Pamoja na vikao hivyo kamati ndogo mbalimbali za shughuli hiyo ya uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru zinaendelea na majukumu yake kuhakikisha siku hiyo shughuli zinafanyika kama ilivyopangwa kwa kiwango na ufanisi mkubwa.
Pamoja na shughuli hizo pia maandaliza ya halaiki yanaendelea kwa walimu na wakufunzi kuendelea na mafunzo kwa watoto watakaoifanya siku hiyo kufana  kwa ustadi mkubwa ambao wataupata kutoka kwa wataalam wa shughuli za halaiki.
Wananchi wa Mkoa wa Kagera na nje ya mkoa wa Kagera mnaalikwa kufika siku hiyo ya uzinduzi wa Mbio za mwenge wa uhuru hapa mkoani Kagera katika uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba ili kujionea tukio hilo la kihistori na kumbukumbu kwa mkoa wetu na taifa kwa ujumla.
Tukio hilo si la kukosa  kwani Mwenge wa Uhuru huleta nuru penye giza, huleta amani penye mfarakano,Mwenge wa Uhuru pia hueneza huleta upendo na mshikamao ndani ya wananchi kwa kuwaunganisha na kuwaleta pamoja.
Wanakagera tudumishe mshikamano na upendo na ukarimukwa kipindi chote ambacho tunatarajia kupokea wageni mbalimbali wa kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha wanafika mkoani kwetu kuhudhuria uzinduzi na kuondoka kwa amani.
Pia kama ilivyo kawaida yetu Wanakagera kuuweka mkoa wetu safi  kila mara tunakumbushwa kuendelea na utaratibu huo na kuhakikisha kuwa maeneo yetu yanakuwa safi nay a kuvutia kama ilivyo siku zote ili kuufanya uzinduzi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka huu kung’ara  zaidi.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014
Next Post Previous Post
Bukobawadau