Bukobawadau

MWENDELEZO YANAYOJILI BUNGENI HOTUBA YA RAIS UZINDUZI WA BUNGE MAALUM LEO MARCHI 21,2014


Naaam sasa Rais JK anaingia Ukumbini kwa kupitia ule mlango wa VIP

- Mheshimiwa Abeid Amani Karume sasa Anaingia

- Mzee Ruksa, Ali Hassan Mwinyi anaingia sasa

- Jaji Mkuu wa Zanzibar, Jaji Makungu anaingia Bungeni sasa

- Jaji Mkuu, Mohamed Chande aorhman anaingia sasa

- Makamu wa Kwanza wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad anaingia ukumbini

- Anayefuata ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Mohamed Shein

- Anayefuata ni Makamu wa Rais, Dr Mohamed Ghalib Bilal

- Wageni wote muhimu wamewasili na sasa anayesubiriwa ni Mheshimiwa Rais kuingia Bungeni

- Naam mzee wa Speed and Standard anamsindikiza Rais JK kuingia ukumbini. Mayowe yanapigwa kuashiria furaha ya wabunge. Namuona mheshimiwa mnyaa anapiga meza muda wote

- Mzee Malecela naye yumo. Pia kuna Pius Msekwa, mama Maria Nyerere na wake za viongozi

- RAIS KIKWETE ANAANZA KUHUTUBIA KWA KUCHEKA NA KUSEMA:"haijapata kutokea". Sijui ana maana gani...

- Rais anawaponyeza Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti kwa kuchaguliwa kwa kishindo. Anawapongeza pia wabunge kwa fursa hii waliyopata ya kuwa wabunge wa bunge la katiba. Anasema kuwa wabunge watatunga katiba inayokubalika na watanzania, inayotekelezeka, itakayoondoa changamoto za muungano zilizopo, itakayoimarisha muungano, itakayodumisha amani na usalama, itakayostawisha demokrasia, kuimarisha utawala wa kisheria, kupunguza maovu, kukuza uchumi na kuleta maendeleo sawia kwa wananchi

- Rais anasema kuwa hii ni mara ya Tatu Tanzania kuandaa katiba. 1965, 1977 na huu wa sasa. Ila anasema huu wa sasa unashirikisha wananchi kwa kutoa maoni yao, mabaraza ya katiba na kwa kura ya maoni. Tofauti na michakato iliyotanguloa ambapo ni wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano tu, mchakato wa sasa una wengi na unashirikisha makundi mengi

- Rais anasema kuwa kelele za kutaka kuwa na katiba mpya zimekuwepo sana wakati wa mfumo wa vyama vingi

- Anampongeza jaji Warioba na wajumbe wote wa tume.

- Suala la mawaziri kutokuwa wabunge nalo anataka litafakariwe kwa makini. Anawataka wajumbe watafakari kwa kina kuhusu hilo. Kwamba lina uzuri na ubaya wake

- Sasa anajadili kuhusu muundo wa Muungano. Anasema kuwa jambo hili limezua mjadala mzito tangu Rasimu ya mwanzo hadi ya mwisho. Anasema kuwa jambo hilo linasubiriwa kwa hamu na watanzania wengi. Karika hilo anaroa ushauri ufuatao

    Wabunge waepuke jazba wakati wa kujadili suala hilo
    wajumbe watafakari madhara yanayoweza kujitokeza iwapo jambo hilo halitapatiwa ufumbuzi kwa njia ya utulivu
- Anasema kuwa mjadala wa muundo wa katiba moya si mheni kama alivyoeleza Warioba. Kwamba mwaka 1984 ulikuwa chanzo cha machafuko Zanzibar. Pia mwaka 1993 jambo hilo lilikuwa ni chanzo na G55

- Rais Kikwete anasema kuwa sababu za kuwa na serikali mbili ni mbili

    Kuhakikisha kuwa Zanzibar haimezwi kwenye Muungano
    kuepuka gharama kwa Tanzania Bara kugharamia serikali ya bara na ya muungano

- Rais anasema kuwa kwa mujibu wa Jaji Warioba ni Muundo wa serikali Tatu, umependekezwa kutokana na sababu mbili.

    Kwamba watanzania wengi wamependekeza muundo huo
    unatoa majibu ya matatizo ya serikali mbili
Next Post Previous Post
Bukobawadau