Bukobawadau

SOMO KWA VIONGOZI NA WANACHAMA WA CCM JIMBO LA KALENGA.KUTOKA KWA MANGULA

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akionyesha mfano wa karatasi la kupiga kura kwa wanachama wa CCM wanaoishi kwenye kitongoji cha Ulete,Kijiji cha Muwimbi mkoani Iringa.
 Mgombea wa kiti cha Ubunge jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM Ndugu Godfrey Mgimwa akiomba kura kwa wakazi wa kitongoji cha Ulete ,kijiji cha Muwimbi mkoani Iringa ambapo aliwaambia tusikilize sera za kuleta maendeleo na si porojo zisizo na tija kwa Taifa letu. 
 Katibu wa UWT CCM Arusha mjini Ndugu Rehema Mohamed akiwahutubia wakazi wa kitongoji cha Ulete kijiji cha Muwimbi na kuwaambia Mgimwa atasukuma maendeleo ya Jimbo hilo na atakuwa muwakilishi mzuri wa jimbo hilo kwa wananchi Bungeni na kwa madiwani.
 Baadhi ya Viongozi wa CCM kata ya Ifunda wakiangaia mfano wa karatasi la kupigia kura ambapo wameshauria kusimamia watu wao kushiriki kupiga kura siku ya tarehe 16 March 2014.

 Mwakamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akihutubia viongozi na Mabalozi 26 wa CCM waKata ya Ifunda,kijiji cha Mfukulembe ambapo aliwasihi kuwa makini na zoezi zima la upigaji kura na kutupilia mbali kauli za vyama pinzani zinazosema zitalinda kura kwa helkopta kwani kila chama kinatoa wakala wake wa kusimamia wakati wa zoezi la kupiga kura.Makamu Mwenyekiti CCM (Bara) aliendelea kuhutubia bila kujali mvua.
 Godfrey Mgimwa mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la Kalenga kupitia CCM akihutubia viongozi na mabalozi 26 wa CCM wa kata ya Ifunda kijiji cha Mfukulembe na kuwaambia kwa kutumia ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo atavipa kipaumbele elimu, afya , na ujenzi wa barabara.
Next Post Previous Post
Bukobawadau