Bukobawadau

SOKA (MPIRA WA MIGUU)HUKO KASHARUNGA MULEBA

Diwani Kata ya Kasharunga wilayani Muleba Alhaji Khalid Hussen akigawa zawadi kwa mshindi wa ligi ya Diwani,kama ilivyokuwa azma yake  ambapo Kasharunga FC mshindi wa kwanza Kasharunga Fc wamepata Tsh.100,000/- na mpira,Mshindi wa pili  Runazi kupata 75,000/-Mshindi wa tatu Nyakachuro FC walipata Tsh 50,000 na kila timu shiriki ilipewa Tsh.15 000/-na mpira wa miguu mmoja ambapo  gharama ya uendeshaji na vifaa vya michezo kwa timu nane zilizoshiriki vilifikia thamani ya Tsh 2.5mil.
 Diwani Kata ya Kasharunga wilayani Muleba Alhaji Khalid Hussen akigawa vifaa vya michezo kwa timu zilizoshiriki ligi yake
Na Shaaban Ndyamukama
MULEBA: Ligi ya diwani kata ya Kasharunga  wilayani Muleba Mkoani Kagera juzi imemalizika hatua ya kuchezwa fainali baada ya timu ya Kasharunga kuibuka  kidedea dhidi ya Runazi Stars ya katani humo kwa kuichapa bao 1-0

Tangu kuanza kwa mchezo huo timu zote zilishambuliana kwa nguvu lakini hakuna mchezaji aliyeweza kuwaona  walinda milango kutikisa vyavu za timu pinzani licha ya kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu na kutangazwa kupitia vipaza sauti.
Katika fainali hiyo timu hizo zilicheza bila kufungana katika dakika 90 na kwenye dakika 30 za nyongeza ndipo kasharunga walifunga kupitia kwa  Mudasiri Hemed ambapo licha ya goli hili  kuingia wachezaji wa  timu ya Runazi  hawakuridhika
Katika  kuimarisha mahusiano ya kimichezo diwani wa kata hiyo Alhaji Khalidi Hussen alishauri mpira huo kuisha na kugawa zawadi kama ilivyokuwa azma yake  ambapo Kasharunga FC kuipatia Tsh.100,000/- na mpira  Runazi kupata 75,000/-
Mshindi wa tatu Nyakachuro FC walipata Tsh 50,000 na kila timu shiriki ilipewa Tsh.15 000/-na mpira wa miguu mmoja ambapo  gharama ya uendeshaji na vifaa vya michezo kwa timu nane zilizoshiriki vilifikia thamani ya Tsh 2.5mil.
Alhaji Khalidi Hussen kabla ya kukabidhi zawadi hizo alisema kuwa lengo la kuekwa kwa ligi hiyo ni kuwaweka vijana kuwa pamoja na kujenga mahusiano ya karibu ili hatimaye wajiunge pamoja kuanzisha miradi ya ujasiliamali
Alisema vijana wengi wanashindwa kujikomboa kimaisha na kubaki tegemezi ana ombaomba kwa kile alichokiita kubweteka na kujadili maisha ya wanasiasa na majukumu yao bila wao vijana kujiendeleza kwa kuwa na miradi ya maendeleo
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili katika kata hiyo  wakiwemo makocha watimu mbalimbali walisema mzunguko wa ligi ulikuwa ni wa kusisimua na kuwaweka watu katika hali ya furaha burudani na na amani
Pamoja na hayo refa wa mchezo huo aliyetambulika kwa jina la Maximilian Yusuph  na kocha wa Runazi stars Jackso Tibalibusha nao walidai licha ya mchezo huo kuwa na ubishi wakati wa fainali bado unawajengea umoja.
Next Post Previous Post
Bukobawadau