Bukobawadau

SHUGHULI YA MAZISHI YA MAREHEMU DENIS RWEHABURA MBEKENGA ILIYOFANYIKA KIJIJINI KAMISHANGO-OMUKIGANGO WILAYANI MULEBA JIONI YA LEO APRILI 17,2014

Ibada takatifu katika shughuli ya mazishi ya Marehemu Denis Rwehumbiza Mbekenga, iliyofanyika Nyumbani kwao kijijini Kamishango- Omukigando Wilayani Muleba mkoani Kagera. CHECK SEHEMU YA KIPANDE CHA VIDEO KATIKA MAZISHI YA MAREHEMU DENIS RWEHABURA MBEKENGA
Marehemu Denis Mbekenga pichani amefariki tarehe 12.4.2014  katika hospital ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam,akiwa na umri wa miaka 48 ilikuwa saa 1.00 jioni siku ya Jumamosi.
 Ndikagya Omwiguru (Nitaenda Mbuguni) ni ni wimbo wa dini wa kilugha ambao  Marehemu Denis Rwehumbiza Mbekenga aliupenda sana katika maisha yake ya kuishi.
 'Ntaenda mbinguni 'tunaomba wadau wasomaji wetu tumsindikize Marehemu Denis  Rwehumbiza  Mbekenga kwa wimbo huo alio upenda akiwa masomoni na hii ni kutokana na kile tulichokishuhudia  jioni ya leo katika shughuli ya mazishi yake
 Wakati shughuli ya Ibada ya mazishi ikiendelea, Bukobawadau tunakupatia mistari ya wimbo 'Ndikagya Omwiguru, ndikagya Omwiguru, Ndibona Maria.
1. Ndigya ndimubona, mbone mawe Maria, Omwiguru lya Mungu n'Abatakatifu.
 2.Ndigya ndimubona, Nyin' Omukama wange, tuliba ntukurata n'Abatakatifu
3.Ndigya ndimubona, ndiba hao na mawe, byona ebyo ndikwetaga arabimarila
 4.Ndigya ndimubona,nyinaichwe omurungi, ndishemelelwa nawe amakiro gona.
5. Ndigya ndimubona, tugendane ichwena, maweichwe natwetaga,tugye kumuleba.
6. Kugya kumubona, amagezi ti gangi, tumwesige wenene aratujunaga,'Ni maneno ya wimbo wa dini  katika lugha ya kihaya '
Maneno yaliyomo katika kutafsiri Bibliailiyotafdiriwa  katika Lugha ya Kihaya ambayo inatumika hadi leo hii
Taswira mbalimbali katika shughuli ya mazishi haya,Picha zaidi za Matukio ya shughuli hii zinapatika katika ukurasa wetu wa facebook.
 Pichani ni watoto wa Marehemu na Mjane wa Marehemu Denis Mbekenga,Bi Rose Denis Mbekenga
Ibada ya mazishi ikiendelea.
 Sehemu ya Waombolezaji wa Msiba wa Marehemu Denis Mbekenga.


Kwa Umati huu unojionyesha ,basi utakubaliana nasi juu ya kile tulichokisema mapema
 Taswira kamili wakati shughuli ya Ibada ya mazishi ikiendelea.
 MAISHA YA KIROHO;Marehemu Denis Mbekenga katika maisha yake alifanikiwa kupata Sacramenti tatu kati ya Saba.
 Marehemu alibatizwa mwaka 1966 na kupata Sacrementi ya Ekaristi mwaka 1979 katika kanisa la Kamishango,Mwaka 1984 alipata Sacramenti ya kipaimara(Comfirmation)akiwa seminari ya Rubya.
TAALUMA;Marehemu alianza shule ya msingi Kamishango mwaka 1976 na kumaliza darasa la tano mwaka 1980,Mwaka 1981 alijiunga na Seminari ndogo ya Rutabo iliyopo Wilayani Muleba na kuhitimu darasa la Saba mwaka 1982.
 Mwaka 1983 Marehemu Denis Rwehumbiza Mbekenga alijiunga na Seminari ya Rubya na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1986.
 Mwaka 1987 alijiunga na Shule ya Sekondari ya Sangu katika Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na sita na kuhitimu mwaka 1989 katika masomo ya uchumi Hisabati na Jiografia.
 Wasifu wa malehemu unaendelea kusema; Mwaka 1989 alijiunga na Jeshi la kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria katika kambi ya Maramba Mkoani Tanga.
 Mwaka 1992 Marehemu Denis alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada ya kwanza katika fani ya sanaa ya TAKWIMU na kuhitimu  mwaka 1995.
Marehemu Denis Mbekenga alijiunga tena na chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1998 na kuchukua shahada  ya pili katika fani ya Utawala/Uongozi wa Biashara na kuhitimu mwaka 1999.
Ndugu wa familia wakishiriki Ibada ya Mazishi
 Mzee Emmanuel Mbekenga, Baba Mzazi wa Marehemu Denis akitoa heshima ya mwisho kwa mwanae.
Itican D. Mbekenga, mtoto wa Marehemu akishuhudia mwili wa Baba yake.
Mama Angelina Emmanuel Mbekenga, mama mzazi wa Marehemu Denis Mbekenga.
Bi Rose, mjane wa Marehemu mara baada ya kushuhudia Mwili wa mmewe.
 Watu kadhaa walianguka na kupoteza fahamu wakati wakiwa katika zoezi la kushuhudia mwili wa Marehemu Denis Mbekenga, pichani ni mjane Bi Rose Denis Mbekenga.
 Leticia Nchwal Mbekenga, Dada wa Marehemu Denis Mbekenga.
Ni huzuni mkubwa kwa ndugu na familia ya Marehemu Denis Mbekenga.
 Ilibidi nguvu za ziada zitumike wakati mmoja wa wanafamilia akiubusu mwili wa Marehemu.
Zoezi la kuuaga mwili wa Marehemu Denis Mbekenga likiendela.
 Baadhi ya waombolezaji wakishuhudia Mwili wa Marehemu.
 Picha ya Marehemu Denis Mbekenga
 Sehemu ya waombolezaji.
Ibada ya mazishi ikiwa inaendelea.
  Jeneza lenye mwili wa Denis Mbekenga likiwa tayari eneo la kaburini
 Jeneza likishushwa kaburini
 Sisi tu mavumbi,na mavumbini tutarudi.
 Padri akiongoza zoezi la kuweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Denis Mbekenga.
 Mzee Emmanuel Mbekenga, Baba Mzazi wa Marehemu Denis Mbekenga akiweka shada la maua kaburini.
 Mjane wa Marehemu akisogea katika Kaburi la mumewe.
 Wakati zoezi la kuweka mashada ya maua kaburiniukiendelea....
 Anaonekano Mdau Alex Mtiganzi pichani katikati.
Dada wa Marehemu Denis Mbekenga katika zoezi la kuweka mashada ya maua kaburini.
 Waombolezaji wakishiriki katika mazishi.


Shughuli mazishi inaendelea katika eneo la makaburi yaliopo nyumbani kwa mzee Emmanuel , Omukigando-Kamishango kama inavyo onekana pichani  mamia ya watu wameweza kuhudhuria maziko haya.
Sehemu ya Wadau walioshiriki  katika shughuli ya mazishi haya.
Sisi sote ni waja wa M/MUNGU na sote tutarejea kwake,Bukobawadau Blog tunamuombea  kwa Mwenyzi Mungu ampokee na amsamehe marehemu Denis  makosa yake
 Neno kutoka katika Ofisi , marehemu aliyofanyia kazi.
 Utaratibu kutokoa kwa muongozaji wa shughuli hii.
Ndugu Felix Mbekenga akisoma wasifu wa Marehemu Denis Rwehabura Mbekenga ambapo Marehemu aliishi maisha ya ndoa toka mwaka 2000 hadi umauti unamchukua, ameacha mke na watoto watatu, wawili wa kiume na mmoja wa kike.
 VIDEO  ya mazishi haya  itapatikana 
Wakazi wa Omukigando Kamishango waliojitokeza katika Mazishi haya.
Bukobawadau Blog tunatoa pole kwa familia ya marehemu Denis Rwehumbiza  Mbekenga  kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi.

Next Post Previous Post
Bukobawadau