Bukobawadau

TASWIRA KAMILI UWANJANI BAYERN 3-1 MAN UNITED (4-2 agg)

Timu ya  Manchester United imetolewa  nje katika mashindano  ya Ligi ya Mabingwa baada ya kushindwa kuonyesha cheche dhidi  Bayern Munich.
 Rooney na Dante wakiruka juu kwa pamoja, hii ni mwanzoni mwa mchezo.
Mwiba katika upande:Mchezaji waArjen Robben pichani (kulia) akizungusha mpira kwa nyuma na kuufuata mbele ya Darren Fletcher ,kinyumbani tunasema kujitangulia.!!
Mara kadhaa ameonekana Mchezaji wa Manchester United Danny Welbeck  akijikwatua visigino yeye mwenyewe, maelekezo haya aijulikani kayapata kwa wapi?na lengo lake ni nini?
Sintofahamu wakati nahodha wa Manchester United anapata kadi ya Njanoa pale alipomchezea vibaya Mchezaji Mandzukic.
Hekaheka uwanjani.

Mipango kati Wayne Rooney pichani  (kulia) na Patrice Evra kama wanavyo onekana wakijadiliana

Mabadiliko ya Tactical:Kocha wa Buyern Guardiola akitoa maelekezo ya kubadili mfumo kwa wachezaji wake
Yawezekana huu ukawa ndio mwisho wa Kocha David Moyes.




Ikiwa ni dakika ya 62, hii ni Moja ya nafasi muhimu kwa Wayne Rooney baada ya kupokea pasi nzuri  kutoka kwa Danny Welbeck,Wahaya wanamsemo wao'atakushutulile ati teneka' maswali ni mengi juu ya Rooney kwani nafasi nyingi hakuweza kuzitendea haki.
Hekaheka uwanjani hakuna aliyejua kuwa Nyota inaweza kumuakia  Patrice Evra
Shangwe za muda  mchache kwa Mchezaji Patric Evra baada ya kutupia bao la kuongoza.
Harakati za David de Gea ni kuzuia bao la  Mandzukic lililopelekea Ubao kusomeka 1-1
Anaonekana Mario Mandzukic baada ya kusawazisha bao kwa Bayern Munich ikiwa ni sekunde 22 tu baada ya Patrice Evra
Noma ni kwamba bao la manchester Unated limedumu kwa sekunde 22 tu!!Sasa ni 1-1
 Thomas Muller anaipatia  Bayern bao la pili la kuongoza BAYERN 2-1 Man United (Muller 68).
Bao la 2 la Buyern  kupitia kwa Thomas Muller pale alipokitumia vyema kichwa chake na kuwaacha wachezaji wa Man U katika hali hii pichani
 Licha ya kuwepo deflected, wakati mchezaji  Arjen Robben anachukua maamuzu sahii,kwa shuti kali lenye kasi binafsi ninachoweza kusema siku ya leo olikuwa dhahama kwa Manchester United
  Hakuna mchezaji mtata ndani ya 18 kama Arjen Robben , kama mdhaa vile ndani ya 18 ghafla macho yangu yanashuhudia kile nilicho kitalajia kwani haikuwa kazi rahisi  kwa kipa wa Man U,De Gea .BAYERN 3-1 Man United (Robben 76
 Bayern wanaendeleza kasi kupitia kwa Mchezaji Robben na kumuacha kipa David De Gea akiwa ameshika kiuno.
 Ubora wa mchezaji ni pale mchango wako unapo onekana katika mechi ngumu na muhimu:Arjen Robben Robben akionyeshaa utukufu wake mbele ya mashabiki wa Bayern
 'Pamoja na juhudi zetu zote kiukweli Bayern wamekuwa kitu kingine ndani ya dakika 20 toka tulipotangulia  kuwafunga kupitia kwa Patrice Evra imekuwa shidaaaaa!!!' Rooney
 Ahhh ni baada ya Carrick kukosa utulivu pale alipopata nafasi ya wazi mnamo dk ya 84 ya mchezo baada ya shuti lake kuonekana fyonga kwa kuelekea  juu kabisa.
Dakika ya 88 ya mchezo!Mchezaji  Claudio Pizarro aliwainua mashabiki wa Bayern Munich juu,lakini juhudu zake za kupata bao la nne zimezimwa na mlinda mlango De Gea wa Man U
Anaitimisha kazi muamuzi  Katika uangalizi: Swede Jonas Eriksson kutoka Sweden.
Next Post Previous Post
Bukobawadau