Bukobawadau

UBELGIJI WATEKETEZA TANI 1.5 ZA MENO YA TEMBO

Picha inaonesha meno ya tembo na Mtambo wa kuteketeza meno hayo. Leo hii Serikali ya Ubelgiji imeteketeza meno ya tembo tani 1.5 iliyoyakamata yakiingingizwa Ubelgiji. Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala  ameipongeza Serikali ya Ubelgiji kwa hatua hiyo na ameziomba nchi nyingine zenye soko la meno hayo kuchukua hatua kama ilivyofanya Serikali ya Ubelgiji. Aidha, Balozi Kamala ameziomba nchi zilizoendelea kusaidiana na nchi zinazoendelea kupambana na ujangiri.
Next Post Previous Post
Bukobawadau