Bukobawadau

MATUKIO YA MWENGE WILAYANI NGARA

 Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu akikiri kupokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Karagwe Dary Rwegasira  katika kijiji cha kasulo wilayani Ngara.
Dc ngara akipokea mwenge kutoka kwa DC wa karagwe
 Mkuu wa wilaya ya Karagwe Dary Rwegasira akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu katika kijiji cha kasulo wilayani Ngara
 Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mt.Alfred Rulenge wilayaniu Ngara wakigusa na kupokea mwenge wa uhuru ulipotembelea shule hiyo kuzindua shambala miti 12mil katika mashamba matatu ya shule hiyo
  Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mt.Alfred Rulenge wilayaniu Ngara wakigusa na kupokea mwenge wa uhuru
 Mwenge umekabidhiwa kutoka wilayani Karagwe na mkuu wa wilaya hiyoa Dary Rwegasira aliukabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu eneo la Benako kata ya Kasulu wilayani Ngara majira ya saa 2asubuhi ya leo
 Mara baada ya kuupokea Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Kanyasu alisema ukiwa wilayani kwake utazindua kukagua kfungua na kuweka mawe ya msingi miradi saba yenye thamani ya shilingi Bil 1 na milioni 213
 Alisema miradi hiyo ni katika sekta ya maji eneo la Benaco kilimo kwenye shamba la migomba la Samweli Kapalala, Kuzindua Kibanio cha Mifugo Nyakisasa (Tsh 12mil) na kuweka jiwe la msingi Kituo cha Afya kijiji cha Kashinga  kata ya Nyakisasa
Aidha alisema mradi mwingine ni hifadhi ya mazingira katika shule ya sekondari Rulenge  ambayo imepanda miti 12mil  na malengo ni kufikisha miti 30mil ambapo kila manafunzi hupanda miti 5 kwa kila mwaka
Pamoja na hayo mwenge huo umezindua jengo la utawala katika Shule ya sekondari ya Rhec English Medium kata ya Rulenge  na hatimaye kutoa cheki ya mikopo sacos ya vijana mjini Ngara
Mkesha wa mwenge umefanyika katika viwanja vya posta ya zamani mjini Ngara na utakabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Biharamulo Richard Mbeo katika kijiji cha Nyabugombe kata ya Nyakahura .
Next Post Previous Post
Bukobawadau