Bukobawadau

WAKIMBIZA MWENGE WAZAWADIWA MIKUNGU YA NDIZI -NGARA

 Kaimu kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Hamza Muhamudi akikata mkungu wa ndizi katika shamba la  migomba la Samweli Kapalala (Kulia kwake) katika kijiji cha Kasulo Wilayani Ngara mkoani Kagera baada ya kupewa kama zawadi
 Watanzania wametakiwa kutumia ardhi kama rasilimali   ya kujikwamua kiuchumi kwa kufanya kazi kwa bidii na kunufaika na matunda yanayopatika baada ya kuzalisha mali kupitia miradi ya kilimo na mifugo kujipatia maendeleo
Kaimu kiongozi wa mbio za mwenge  wa uhuru Kitaifa Hamza Mohamudi ametoa wito huo jana wakati akikagua shamba la mkulima wa zao la ndizi katika kijiji cha Kasulo wilayani Ngara mkoani kagera
Kaimu kiongozi wa mbio za mwenge  wa uhuru Kitaifa Hamza Mohamudi ametoa wito huo jana wakati akikagua shamba la mkulima wa zao la ndizi katika kijiji cha Kasulo wilayani Ngara mkoani kagera 
 Muhamud amesema licha ya wakulima wa migomba mkoani kagera  kushambuliwa na ugonjwa wa  unyanjano na kukosa  chakula kwa kutumia utaalamu wa kisasa na kilimo bora ugonjwa huo unaweza kutokomea haraka
 Amesema kitendo cha mkulima kutumia mtaji wake wa ardhi  na mifugo kidogo kuandaa shamba na kutoa mazao yenye soko katika wilaya nzima na mkoa ni jambo la kuigwa katika uchu wa kujiletea maendeleo ya familia wilaya na mkoa
Aidha amempongeza mkulima wa migomba Samweli Kapalala ambaye shamba lake alilianzisha mwaka 2003 kwa kianzio cha ekari mbili  ambapo sasa limefikia ekari 6.5 likiwa na miche au mashina 444 ya migomba.
 “Ndugu yangu sinabudi kukushukuru kwa jitihada na nguvu kazi unayotumia katika shamba hili na vijana uwarithishe kwa kuwaelekeza mbinu na mtaji ulioanza nao ili waondokane na umaskini”.Alisema Mohamudi
Akitoa taarifa za mradi wa shamba hilo Samweli Kapalala  alisema katika shamba hilo  hupanda migomba inayotoa ndizi aina ya Nchakala  na sehemu ya shamba amepanda migomba aina ya FIA 17& 23 kwa kutumia wataalamu wa kilimo
Alisema mkungu wa ndizi unauzwa kati ya Sh 15,000/-kwa aina ya Nchakala na Sh 35,000/ kwa ndizi aina ya FIA 17& 23 ambapo katika faida aliyokwisha pata ni kusomesha watoto kununua ng’ombe  kupata mbolea na amejenga nyumba bora
“Natumia shamba hili kufundishia wakulima wa ndani na nje ya nchi   na  shamba hili limeniwezesha kuwa mshindi wa kwanza kimkoa mwaka 2012 na wa pili kwa mwaka 2013 katika  maonesho ya nanenane kikanda”.Alisema Kapalala
Pamoja na faida hiyo alisema tangu kuanzishwa kwa shamba hilo hadi sasa lina thamani ya Sh250,000,000 lakini katika uzalishaji zimeshapatikana Sh 375 mil ingawa changamoto ni ukosefu wa soko na ugonjwa wa unyanjano 

NGARA: Na Shaaban Ndyamukama
Next Post Previous Post
Bukobawadau