Bukobawadau

MTOTO WA PELE JELA MIAKA 33

Mwanawe gwiji wa soka Brazil na duniani kote, Pele, Edinho Pele, amefungwa jela miaka 33 kwa kufanya biashara haramu ya pesa au kujipatia pesa chafu zilizotokana na biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya.
Edinho ni mchezaji soka mstaafu, aliyecheza kama mlinda lango katika klabu ya Santon aliyowahi kuchezea Pele mapema miaka ya tisini.
Alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na kutumikia kifungo kwa kosa la ulanguzi wa dawa za kulevya pamoja na kuwa na uhusiano na mlanguzi sugu wa dawa hizo mjini Santos.
Edinhio, alikiri kosa la kuwa mraibu wa dawa za kulevya lakini alikanusha madai ya kuhusika na ulanguzi wa dawa hizo.
 Pele alimtembelea mwanawe Jela
 Uamuzi wa mahakama ulitolewa mjini Praia Grande, katika jimbo la Sao Paulo.
Vyombo vya habari nchini humo bado havijaweza kupata kunena na Edinho, ambaye jina lake halisi ni Edson Cholbi do Nascimento, lakini vinasema kuwa huenda akakata rufaa.
Edinho, mwenye umri wa miaka 43, alikuwa mlinda lango wa Santos.
Pele, au kwa jina lengine, Edson Arantes do Nascimento, alisakatia soka yake nchini Brazil , na kuwakilisha Brazil katika kombe la dunia mwaka 1958, 1962 na 1970 na kupata sifa ya kuwa mchezaji bora katika kizazi chake.
Pele mwenye umri wa miaka 73, alishinda kombe la dunia mara tatu akichezea Brazil na kuingiza zaidi ya mabao 1,200 katika historia yake ya kucheza.
Alistaafu mwaka 1974, lakini akaanza kucheza tena mwaka mmoja baadaye mjini New York Marekani.
Edinho ni mtoto wa tatu wa Pele kutoka kwa ndoa yake ya kwanza
Next Post Previous Post
Bukobawadau