Bukobawadau

PICHA TATA ZA DIAMOND NA WEMA ZATINGA MJENGONI

Staa Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kwenye pozi lenye utata.
 Stori: Mwandishi Wetu
Sakata la mastaa wakiwemo Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ kupiga picha chafu kisha kuzitundika mitandaoni limetinga bungeni baada ya juzikati baadhi ya wabunge kulishupalia.

Hilo liliibuka Suzi mjengoni katika kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Saidi Mtanda alitaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tabia za watu maarufu kupiga picha zisizo na maadili kisha kuziweka mtandaoni.
Katika kujibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alisema: “Tunajitahidi kuhakikisha wanaofanya hivyo wanachukuliwa hatua stahili ili kukabiliana na matendo hayo ambayo ni kinyume na maadili.”
 Mastaa Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakiwa kwenye pozi la kimahaba
 Katika kuonesha kutoridhika na majibu ya waziri, Mheshimiwa Mtanda alipopewa nafasi aulize swali la nyongeza alisema: “Mheshimwa spika nahisi swali langu halijajibiwa ipasavyo. Nilichotaka kujua ni hatua ambazo zimechukuliwa kwa baadhi ya watu mastaa kama vile Wema na Diamond ambao hupiga picha zao zisizofaa kisha kuziweka mtandaoni.”
Kufuatia swali hilo, Nkamia alisimama na kujibu kwamba, serikali imeweka mikakati na njia sahihi za kukabiliana na tabia hiyo na kwamba wale ambao watabainika watachukuliwa hatua zinazostahili.
 Licha ya majibu hayo, bado wabunge walionesha kutoridhika, hali ambayo Spika Anne Makinda aliiona na yeye akaongezea “Waheshimiwa wanataka kujua na za hivi karibuni zilizovuja mtandaoni” ambapo jibu la Nkamia lilikuwa:
“Mheshimiwa kuhusu hizi picha za juzi zilizosambaa mtandaoni, tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila tutachukua hatua tutakapobaini zilikotokea.”
Next Post Previous Post
Bukobawadau