Bukobawadau

ZIARA YA PROF.TIBAIJUKA JIMBONI

 PROFESA TIBAIJUKA akikagua darasa la elimu ya awali katika shule ya msingi katanda  ambalo liko hali mbaya kwa kukaribia kuanguka ambapo ameahidi kujenga darasa  jipya la kisasa kwa wananchi kuchangia vifaa vinavyopatikana kwenye mazingira yao na nguvu zao
MBUNGE wa jimbo la Muleba kusini Profesa Anna Tibaijuka ameahidi kujenga  madrasa matatu katika shule yamsingi Katanda na Kyamate  wilayani Muleba  baada ya kukuta wanafunzi wa shule hizo kusomea katika madarasa yasiyo  bora.
Profesa Tibaijuka amesema hayo jana wakati alipofanya ziara ya kutembelea shule hizo na kukuta walimu wa shule hizo wanafundishia katika vyumba vya madarasa vilivyo jengwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo kisha kuezekwa kwa bati
Amesema kufuatia hali hiyo atajenga chumba cha elimu ya awali katika shule ya msingi Katanda ambapo wanafunzi 70 wa darasa hilo wanakaa chini katika jengo ambalo limejengwa kwa miti na udongo lakini ni dhaifu hatari kwa maisha yao
Amepongeza  walimu wa shule za msingi   Kyamate   kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na kupata  ufanisi kitaaluma na kuwapatia  Sh500, 000 baada ya shule hiyo kuwa ya 11 kiwilaya katika ufaulu wa darasa la saba mwaka jana

 “Shule sio majengo tu ni pamoja na walimu wenye moyo wa kufanya kazi kwa uzalendo na katika mazingira haya shule hii imezidi walimu wanaojifanya wajanja wa mjini walio na rasilimali na huduma za kijamii”Alisema Profesa Tibaijuka
Amewahimiza wananchi kuchangia vifaa vinavyopatikana katika mazingira yao  hasa mchanga mawe  kokoto na wanawake kuchota maji ili ili kulinda hadhi ya shule hiyo ambayo   ilikuwa ya 11 kati yashule 228 za wilaya ya Muleba
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kyamate Severin Angelo amesema  shule hiyo  ina  wanafunzi 315 wavulana   160 wasichana155 walio katika  madarasa ya muda yaliyojengwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo kisha  kuezekwa  kwa  bati
Amesema kuwa shule hiyo ilianza mwaka 2007  ikiwa na wanafunzi  wa darasa la kwanza  43kati yao  wavulana 25 na wasichana 18 na changamoto kubwa ni kukosekana kwa vyoo ikihiyaji matundu 14 ya wanafunzi na mawili ya walimu.
Naye  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Katanda Suleima Abdalah amesema  shule yake inao wanafunzi 568 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba ikiwa na wanafunzi wa elimu wa awali 70 ambapo ilifunguliwa  mwaka  2004

Alisema  wanafunzi wa shule hiyo wanatumia madawati 70 tu wengine wakika achini  huku walimu saba wa shule hiyo wakitumia  ofisi iliyojengwa na serikali isiyokuwa na meza wala viti na madarasa ya mudani nguvu za jamii
Aidha amesema shule hiyo inahitaji vyoo vya wanafunzi matundu 15 na mawili ya  walimu ambapo wanafunzi wa kiume wanatumia matundu ya muda yaliyo katika hali mbaya kimatumizi na wanafunzi wanatumia matundu yaliyojengwa na serikali .

MULEBA: Na Shaaban Ndyamukama , Mwananchi
Next Post Previous Post
Bukobawadau