Bukobawadau

BONGE LA MECHI UWANJANI KAITABA #MAKIRIKIRI 3-3 BAKOBA #KAGASHEKI CUP 2014

 Siku ya leo Jumapili July13,2014  majira ya Saa 10 Alasiri, kitimtimu cha michuano ya Kombe la Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Mh Balozi Khamis Sued Kagasheki, Imeendelea Uwanjani Kaitaba kwa kuzikutanisha Timu za Bakoba na Kitendaguro.
Picha ya Juu ni Wachezaji wa Timu ya Baboka wakiomba Dua, tayari kwa kuikabili timu ya Kitendaguro Maarufu kwa jina la Makirikiri,picha ya pili ni Sehemu ya Benchi la ufundi
Benchi la Timu ya  bakoba, wa nyuma kabisa  kushoto ni Mh. Diwani wa Bakoba Ndg Bigambo.
 Wakipiga jalamba Uwanjani ni Wachezaji wa Timu ya kata Kitendaguro maarufu kama Makirikiri.
Wachezaji wa MakirikiWakiteta kwa  pamoja katika Duara kama sehemu ya mbinu za kimichezo.
 Mwalimu George, Kocha wa Timu ya Makirikiri timu ambayo mpaka imeshinda mechi zake zote zilizotangulia , ni hatua ya mzunguko michuano ya Kombe la Mbunge 2014.
 Mzee Mwinyi Kocha wa Bakoba Fc.
 Mashabiki wakiendelea kufurahia mechi
 Sehemu ya Mashabiki wa Golani.
 Katikati ni kijina Chichi wa Kapara kama kawaida yeye ni Mhasisi wa Jukwaa hili
 Tayari mpira umeanza , mashabiki wakifuatilia kwa umakini
Meza Kuu yupo Ndg Juma Chama Umande Katibu wa TFF Mkoa,na Ndg Jamal Kalumuna (Jamco)
 Mpira Unaendelea kwa kasi Uwanjani.
Wachezaji wa Makirikiri wakionana kwa kwa pasi za uhakika uwanjani.
 Heka heka zikiendelea Uwanjani
GOAAAALL;Ni Bao la kwanza kwa Timu ya Kitendaguru aka Makirikiri. 1-0
 Mashabiki Jukwaa la Mchanganyiko.
Sehemu ya Wadau pichani wakifuatilia Soka 
 Rama Kachaa katika picha na Rama Sudi, hawa ni Vijana watata  kutoka mitaa ya Kashai Bukoba.
 Bakoba wanapata Penati dakika za mwisho Kipindi cha Kwanza.
 GOAAAll ni bao la kwanza kwa bakoba! ,kipa wa Makirikiri anajaribu kupiga mbizi wakati Si Ukuta anajukuta anachelewa. 2-1
 Mashabiki wa Kitendaguro /Makiriri wakiwa wamenuna
 Wakati ni Shangwe kubwa kwa mashabiki wa Bakoba
 Kipa wa Bakoba katika sintofahamu

Taswira mbalimbali sehemu za mashabiki Uwanjani Kaitaba
 Kipindi Cha pili Timu ya Bakoba wanapata bao la pili la kusawazisha. 2-3
 Uwanja Unalipuka kwa Sangwe kufuatia bao la pili la kusawazisha kwa Bakoba 3-2
 Shangwe za wachezaji wa Bakoba baada ya kupata Bao la pili mnamo dakika ya 80 kipindi cha 2.
 Mdau Sajidu mahaba yanashindwa kujizuia inamladhimu kuwakubali Bakoba
 Mlezi wa Timu ya Bakoba katika ni Uncle Sheby.
 Anaonekana Mh. Ibrabimu Mabrouk wa pili kutoka kulia
 Mchezaji wa Bakoba anafanyiwa madhabi
 Mpira unaendelea, mpaka mwisho#Kitendaguro 3-3 Bakoba
 Mdau Hima Mgonja pichani katikati
 'NakubaliKwamba Hussein Bolt anakimbia balaa ila hawezi kuikimbia njaa';hayo ni maneno kutoka kwa kijana yRama Sudi pichani
 Ni michuano ya Kagasheki Cup 2014, Kabla ya mchezo huu ilitangulia mechi kati ya Kashai na Hamugembe, ambapo kashai waliweza kutowa kichapo cha 4-0 dhidi ya Hamugembe
Kwa hisani kubwa ya ITEMBWE GENERAL SUPPLIES wasambazaji wa ving'amuzi vya Star Times Mjini Bukoba,Star Times wana lengo la kuifanya kila familia ya Afrika iweze kununua, kutazama, na kufurahia zaidi matangazo ya televisheni ya digital kwa muda na wakati sahii
Kampuni ya StarTimes inakubalika na nembo yake inajulikana na kila familia na kwa kila mtu!!!!!



Next Post Previous Post
Bukobawadau