Bukobawadau

CHADEMA NA HARAKATI ZA KUSAKA UBUNGE JIMBO LA NKENGE

 Ndugu Edson Joel Byemelwa,aliyeonesha nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Nkenge Wilaya ya Missenyi  kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA),akiongea na  viongozi wa chama hicho katika kijiji cha Kikukwe,kata ya Kanyigo
Ndugu  Edson Joel Byemelwa akikabidhi vifaa-bendera na kadi kwa Viongozi wa  Chadema Kijijini   Kikukwe.Pichani mwene koti ni katibu  CHADEMA wa kijiji hicho,BwanaVicent Ngaoshwa na mwenye shati la draft  pichani kushoto ni Ndugu Nazari Mukayu,mwenyekiti wa Kitongoji Mwemage -Kikukwe kupitia CHADEMA.
 Baaadhi ya wajumbe katika kikao cha kutangaza nia ya Edson Joel kugombea ubunge wa jimbo la Nkenge
 Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Kikukwe ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Mwemage kupitia CHADEMA,Azari Mukayu,akifafanua jambo wakati wa kumtambulisha Edson Joel kwa wanachama kwa kutangaza nia ya kugombea jimbo la Nkenge

WANACHAMA wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika kijiji cha Kikukwe,kata ya Kanyigo wilayani hapa wamekitaka chama chao makao makuu kufuatilia katika Tume ya Taifa kuhakikisha vijana wote nchini waliofikisha umri wa kujiandikisha kupiga kura, wanaandikishwa ili waweze kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu  ( kama utakuwepo) na uchaguzi mkuu mwakani.

Wanachama hao walitoa rai hiyo mbele ya mwanachama mwenzao,Edson Joel Byemelwa, mzaliwa wa kijiji hicho anayeishi jijini Dar-es –Salaam aliyejitokeza kugombea ubunge wa jimbo la Nkenge la wilaya ya Missenyi.
Akieleza nia yake hiyo Joel alisema vijana wanao wajibu mkubwa kwa nchi yao katika kuleta maendeleo ,hivyo akawataka kujitolea kwani chama chao hakina fedha kama kilivyo chama tawala lakini maendeleo yanayopiganiwa yakipatikana yatawanufaisha wananchi wote.

Aliwaambia wanachama hao kwamba wasisite kuongea na wana CCM na kuwaomba kura kwani wengi wameshachoshwa na chama hicho na wako tayari kuiunga mkono chadema,lakini hawataki kujionesha waziwazi.
Aliwataka wananchi wa kijiji hicho kuunga mkono upinzani kama ilivyo vijiji jirani vya Bugombe na Kigarama na hatimaye jimbo zima kuchukuliwa na CHADEMA katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.Alitoa kadi na bendera kwa kijiji hicho cha Kikukwe.

Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Mwemage kijijini humo kupitia chama hicho.Azari Mukayu aliwataka wanachama kuiga mfano wa kitongoji cha Nyungwe ambapo wanachama wake wengi wakiwa ni vijana hukutana kila mwezi na kuchangia mfuko wao kwa lengo la kuendeleza chama na pia kusaidiana katika shida na raha.

Edson Joel ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na mjasiriamali alisema amepata baraka za chama chake kuwa mmoja wa wagombea ndani ya chama,na yuko kwenye harakati za kuzungukia jimbo kujitambulisha.
 NA MUTAYOBA ARBOGAST,Missenyi
Next Post Previous Post
Bukobawadau