Bukobawadau

TETESI ZA SOKA ULAYA:*Eto'o, Sanchez kwenda Arsenal?*Carvalho kwenda Man U

*Eto'o, Sanchez kwenda Arsenal?*Carvalho kwenda Man U *Adebayor aanza 'kujifua'
Alvaro Negredo anataka kuondoka Manchester City na huenda akarejea Spain. City wamesisitiza kuwa mshambuliaji huyo hauzwi, lakini inafahamika kuwa anataka kujiunga na Atletico Madrid (Daily Mail), Manchester United wameambiwa wanaweza kumsajili kiungo William Carvalho kutoka Sporting Lisbon, lakini lazima walipe pauni milioni 37 kutegua kizingiti cha ununuzi (Daily Express), Everton wamekataa ombi la Tottenham kumsajili beki John Stones (Sun), Southampton wamedhamiria kumshikilia beki wao wa kati Dejan Lovren anayenyatiwa na Liverpool, Tottenham na Arsenal (Daily Express), Juventus wanataka kumchukua beki wa kati wa Man City Matija Nastasic kwa mkopo ili kuziba pengo la Andrea Barzagli ambaye amefanyiwa upasuaji (talksport).
 Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o huenda akasalia EPL- Arsenal na Everton wanafikiria kumchukua (Talksport), beki wa Atletico Madrid Filipe Luis atalazimika kulazimisha uhamisho wake kwenda Chelsea baada ya mazungumzo kati ya timu hizo mbili kudorora (Daily Star), Arsenal na Liverpool watagombea kusaka saini ya nyota wa Chile na Barcelona Alexis Sanchez ambaye huenda akagharimu pauni milioni 30 (Daily Mail), Harry Redknapp amekuwa akizozana na wakuu wa QPR kuhusiana na kutaka kumsajili Rio Ferdinand aliyekuwa Man United (Daily Mirror), Galatasaray wametoa mkataba wa pauni milioni 3 kwa msimu kumshawishi Samuel Eto'o (Le Figaro), Diego Maradona atafanya mazungumzo kuhusiana na kupewa kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Venezuela (Guardian), na hatimaye mshambuliaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor tayari ameanza mazoezi kujiandaa na msimu mpya- na zoezi zaidi analofanya ni mitindo mipya ya kushangilia goli.
Next Post Previous Post
Bukobawadau