Bukobawadau

BOMU LAUA HUKO KIGOMA

Na Mwandishi wetu
WATU watatu wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu katika kijiji cha Migongo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma wakiwa ndani  ya gari la abiria aina ya Hiace.
Akizungumzia tukio hilo leo hii, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilelema, Benedicto  Mahuta, alisema kuwa tukio hilo lilitokea mida ya saa 11 alfajiri ambapo majambazi watano ndio walitekeleza tukio hilo wakati wakiwa kwenye jitihada za kuliteka.
Alisema kuwa awali gari hilo lilikuwa linaelekea Kasulu na lilipofika  katikati ya pori la Kasesema walikuta mtu mmoja amesimama  barabarani akiwa na bunduki ili kusimamisha gari lakini dereva hakusimama, baada ya hatua 15 walikuta mtu mwingine amesimama baada ya kumpita kidogo ndipo bomu likapigwa na kulipuka kwenye gari.
“Kwa mujibu wa dereva wa gari lile,  baada ya bomu kulipuka hakusimama kwa kuhofia kutekwa moja kwa moja  na watu wale hivyo wakaenda kusimama  karibu na kambi ya Jeshi la wananchi na kutoa taarifa ila tayari bomu lile lilikuwa limesha ua na kujeruhi.
Aidha Muhita alisema kuwa Wanajeshi walipopata taarifa walienda  haraka eneo la tukio na walipofika walikuta wale majambazi  walisha kimbia ila wakakuta mwili wa mototo ambaye baada ya bomu kulipuka alitupwa nje ya gari na kufariki.
“Jumla ya watu  waliofariki dunia ni watatu na wengine sita kujeruhiwa, ila majeruhi walikimbizwa katika kituo cha afya cha Muyama, pia baaba ya Jeshi la wananchi kufika eneo la tuki na sisi kufika walitutaka kutoa ushirikiano ili kubaini majambazi wale walikimbilia wapi” aliongeza Muhita
Nae mmoja wa abiria aliyenusulika katika tukio hilo, Agostino Mkuvata  alisema kuwa walipofika eneo la pori walikuta mtu mmoja akiwa ameshika bunduki huku akiielekeza kwenye gari ila kwasababu ilikuwa ni alfajiri na taa za gari zilikuwa zimewaka, dereva alifanikiwa kumpita na walipofika mbele wakamkuta mwingine ambaye baada ya kumpita bomu likapigwa kwenye gari.
“Mwanzo hatukujua kama ni bomu ila tulisikia kitu kimetupwa kwenye gari ila kwasababu mimi nilikuwa nimekaa mbele nilimwambia dereva asisimame  kwa usalama zaidi, ndipo abiria waliokuwa sehemu ya nyumba ya gari wakaanza kupiga kelele kuwa dereva simamisha gari tunakufa” alisema Mkuvaka.
Kwa upande wa Mkuu wa Kituo cha Polisi Cha Wilaya ya Buhigwe, Frank Utonga, alisema kuwa taarifa walishazipata na waliofariki ni watu watatu na majeruhi sita ila hakuna mtu waliomshikilia ila upelelezi unaendelea.
Next Post Previous Post
Bukobawadau