Bukobawadau

KIKAO MAALUM CHA KAMATI YA TAIFA YA MAAFA (TANDREC) CHAFANYIKA LEO, JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa (TANDREC), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka akiongoza Kikao Maalum cha Kamati ya Taifa ya Maafa(TANDREC) ambayo, inaundwa na Washiriki wakuu katika kukabili Maafa, Kikao kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi Dharura na Maafa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Elias Kwesi, akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Maafa (TANDREC) jinsi walivyojidhatiti kuzuia na  kukabili ugonjwa wa Ebola hapa nchini ambapo alibainisha  kuwa hakuna maabukizi ya ugonjwa huo hapa nchini hadi sasa, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka, Kikao kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa (TANDREC) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya kumaliza kikao hicho leo katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam. 
Next Post Previous Post
Bukobawadau