Bukobawadau

BONDIA WA KIKE MWAFRIKA ACHUKUA UBINGWA WA NGUMI ULAYA !

BINTOU YAWA SCHMILL aka "THE VOICE"
Frankfurt,Germany,
Bondia maarufu wa kike mwafrika barani ulaya Bintou Yawa Schmill,mkazi wa Ujerumani siku ya ijumaa 26.September 2014 alifanikiwa kuchukua taji la ubingwa wa ngumi za kulipwa unatambuliwa na IBF,Bondia Bintou alimpiga na kumshinda mpinzani wake bondia Mirjana Vujic   kwa K.O katika raundi ya 3,.
Pambano hilo lilionyeshwa Live katika TV channel ya euro sport na ktazamwa na maelfu ya watu wakishuhudia bondia wa kike mwafrika akirusha ngumi kali kuliko radu.
Bintou Schmill (30) aka The Voice ameshapigana mapambao ya kulipwa 9 na ameshinda 8 kwa K.O,
Katika pambano la Ijumaa 26.September 2014 liliofanyika kwenye ukumbi wa Stadthalle/ Saalbau Frankfurt-Nied,lifanikiwa  kumpa wakati mgumu mpinzani wake kuanzia round ya kwanza hadi ilipofika raund 3 bondia Mirjana Vujickatika alipigwa kwa KO na Bintou Schmill aka "The Voice" kutangazwa ndie bingwa mpya wa uzito wa Welterweight barani ulaya na kuvikwa mkanda huo unatambuliwa na IBF.
Bintou Schmill aka 'The Voice' anaye fananishwa na Simba Jike (Bintou is the Lioness),Simba ambaye ukimuona mpishe njia ulingoni. Bintou "The Voice" Schmill sasa kapania kuweka rekodi ya kuwachapa wapinzania wake kila kona duniani !

Next Post Previous Post
Bukobawadau