Bukobawadau

NGOMA AFRICA BAND YAITAKIA MSONDO NGOMA BAND HERI YA MIAKA 50

 Msondo Ngoma Band kutimiza miaka 50 mwezi Oktoba 2014, Ras Makunja ameitaja Msondo ndio bendi pekee kongwe Afrika !
Bendi maaru ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni almarufu pia kama viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens wenye makao nchi Ujerumani. bendi hiyo inapeleka salam za kuitakia heri ya miaka 50 bendi kongwe barani afrika MSONDO NGOMA MUSIC BAND aka Baba ya Muziki ya watanzania ambayo mwezi Oktoba 2014 itatimiza miaka 50 na kuweka rekodi ya kuwa bendi kongwe pekee barani Afrika !
Kiongozi wa Ngoma Africa band Kamanda Ras Makunja,maitaja bendi ya Msondo Ngoma ndiyo bendi pekee kongwe inayoendelea kutamba tatika medani ya muziki wa dansi barani Afrika na watanzania tuna haki ya kujivunia,
Makunja alisema Msondo Ngoma ilianzisha 1964 kama NUTA Jazz,baadaye kubadili majina kama JUWATA (OTTU) kutoka na wamiliki wa mwanzo Jumuiya ya wafanyakazi Tanzania kubadili majina, na sasa Msondo Ngoma Band aka Baba ya Muziki, kweli ni Baba ya Muziki,maana hakuna bendi kongwe  Afrika zaidi ya Msondo, mfano bendi kongwe kama Orch.Baobab ya Senegal ilianzishwa 1970 haiwezi kuwa kongwe! Zaiko Langa langa (DRC) ilianzishwa 1969 haiwezi kuwa kongwe mbele ya Msondo Ngoma, na T.P OK
jazz ya marehem Franko wa DRC ndio ilikuwa kongwe ilianza 1956 sasa haipo tena,kuna bendi ya Bana Ok ! ya Lutumba Simaroo.
 Ras Makunja alisema Msondo Ngoma band ni ya watanzania lazima tujivunie  Hongereni sana ! baba ya muziki Msondo Ngoma band kwa kuelekea kutimiza miaka 50.
Next Post Previous Post
Bukobawadau