Bukobawadau

SHUKRANI YA MSIBA WA BI STEPHANIA J.KAGANDA

Bw. Deusdedit B. Kaganda kwa niaba ya familia ya Mzee Boniface Kaganda wa Dar es Salaam, anapenda kutoa shukrani kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki katika kipindi chote cha kumuuguza na kushiriki shughuli ya msiba wa Bi. Stephania J. Kaganda, aliyefariki tarehe 12 Agosti na kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele tarehe 15 Agosti 2014, huko kijijini Lukindo, Katoma, Bukoba.

Shukrani za pekee ziwafikie Baba, Mama, Kaka na Dada na watoto wa marehemu kwa kumuuguza  kipindi chote cha kuugua kwake, Bi. Winnie Max, madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera. Dr. Ephraim Kato, madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Mgana, Bukoba  pamoja na Dr. Jean-Pierre Stamm wa clinic ya Medicine Generale FMH, Versoix, Geneva, Switzerland.

Shukrani pia ziwafikie, Majirani na Jumuiya ya Mt. Thomas Acquinas wa Karakata, Airport, Dar es Salaam, Jumuiya ya Kitagata, Lukindo, Katoma, pamoja na Paroko wa Parokia ya Katoma, Bukoba kwa kumjali kipindi chote cha kuugua na kushiriki misa takatifu siku ya msiba.

Shukrani za dhati ziwafikie Katibu Mkuu na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma kwa ushirikiano mkubwa wakati wa kipindi cha kuugua na msiba, Wafanyakazi wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, Geneva, Switzerland pamoja na watanzania wote waishio Uswisi kwa msaada wa hali na mali kufanikisha shughuli ya msiba.

TULIKUPENDA LAKINI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI
Next Post Previous Post
Bukobawadau