Bukobawadau

WATU 115 WALIFARIKI KANISANI NIGERIA

 Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa watu miamoja na kumi na tano wengi wao wakiwa raia wa Afrika Kusini, walifariki baada ya kanisa kuporomoka nchini Nigeria.
Idadi kamili ya raia wa Afrika Kusini waliofariki ilikuwa 84.
Ndege iliyowabeba manusura wa mkasa huo, kumi na sita kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya, imewasili mjini Pretoria.
Zaidi ya watu 300 kutoka Afrika Kusini walikuwa wametembelea kanisa hilo la 'All Nations' mjini Lagos, ambalo linaongozwa na mhubiri T.B. Joshua.
 Muhubiri T.B Joshua amewashangaza wengi kwa kusema aliona ndege ikizunguka jengo hilo kabla ya kuporomoka
Inaarifiwa jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi mbovu.
Mhubiri TB Joshua, amezua wasiwasi baada ya kuzungumzia kuona ndege iliyokuwa inazunguka juu ya kanisa hilo kabla ya jengo lenyewe kuporomoka.
Next Post Previous Post
Bukobawadau