Bukobawadau

BALOZI KAMALA APOKEA VIFAA VYA MCHEZO WA MPIRA KUTOKA CHAMA CHA MPIRA CHA UBELIGIJI

Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa na Viongozi wa Chama cha Mpira cha Ubeligiji baada ya kupokea vifaa vya mchezo wa mpira. Kulia ni Msaidizi wa Rais wa Chama cha Mpira cha Ubeligiji Bwana Thomas Pereira na kushoto ni Bwana Frederic Veraghame Meneja Mwendeshaji wa Chama cha Mpira cha Ubeligiji. Balozi Kamala amepokea vifaa hivyo leo mjini Tubize Ubeligiji. Pamoja na mambo mengine, Balozi Kamala amekubaliana na Viongozi hao kuandaa mpango wa ushirikiano wa kuendeleza mchezo wa mpira kati ya Tanzania na Ubelgiji.
Next Post Previous Post
Bukobawadau