Bukobawadau

MAMIA WAMLILIA KAPTENI MSTAAFU JOHN RWEZAURA BARONGO,WAZIRI WASIRA ASHIRIKI MAZIKO HAYO KIJIJINI KANAZI LEO OCT 25,2014

 Ndivyo anavyowasili kushiriki katika shughuli ya Mazisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe
Wanaonekana Vijana wa Skauti katika utaratibu pembeni ya Mkuu wa Mkoa Mh. Massawe
Taswira Waumini wakiendelea na Ibada.
 Mama Mjane wa Marehemu Kapteni Mstaafu John Barongo.
 Sehemu ya wanafamilia wakati Ibada ya Mazishi ya Maehemu Kapteni Mstaafu John Barongo ikiendelea
 Nyimbo za mapambio ya wakati wa msiba zikiendelea.
 Wapiga Kinanda wakiendelea na mapambio ya nyimbo za kikristo wakati wa Ibada ya Maziko haya
 Padre kutoka Parokia ya Mugana akiongoza Ibada ya Mazishi hayo
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe wakati Ibada inaendelea
 Tukio linalo endelea ni Ibada ya Shughuli ya Mazishi ya Marehemu Kapteni Mstaafu John Barongo Camera yetu ikiwa imejikita vyema kuakikisha unapata kile kilichojiri.
Ibada ya Mazishi ikiendelea .
 Endelea kuwa nasi mpaka mwisho  wa ukurasa huu utapata Video kamili yaliyojiri Jioni ya Oct,25,2014  Shuguli ya Mazishi ya Marehemu Kapt. Mstaafu John Barongo
 Msemaji wa familia Ndg Laurean Rugambwa Bwanakunu akisoma Wasifu wa Marehemu John Rwezaura Barongo
 Mamia ya Wananchi na Viongozi wa Vyama na Serikali washiriki mazishi ya Marehemu Kapteni mstaafu Barongo yaliyofanyika jioni ya leo Oct 25, Kijijini Kanazi-Bukoba Vijijini
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Utaribu Bw Steven Wasira akiongea Kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Serikali
 Bi Jeanifer Mrungi na Mzee Baganda katika hali ya usikivu
 Waziri Wasira  amesema;'Rais Kikwete amemtuma kumwakirisha katika Shughuli hii pia ametuma Salam za rambirambi kwa Familia ya Marehemu Kapteni mstaafu John Barongo kufuatia msiba huu uliotokea  Oktoba 20, 2014 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.'
“Chama kimempoteza mtumishi wake wa muda mrefu na muaminifu, ambaye amefanya kazi zake bila kuchoka na hata baada ya kustaafu amebakia kuwa muaminifu na mwanachama imara,”alisema.
Rais aliongeza kuwa marehemu amekuwa mtumishi hodari katika jeshi, chama na serikali, hivyo mchango wake utathaminiwa siku zote.
 Marehemu Kapteni mstaafu Barongo alizaliwa Desemba 1, 1942 katika kijiji cha Katoja,Wilaya ya Bukoba Mjini mkoani Kagera. Alianza utumishi wake katika Chama cha TANU mwaka 1963 na kuendelea hadi CCM katika mikoa ya Kagera, Kigoma, Mara, Manyara, Shinyanga, Dar es Salaam na Dodoma.
 Mdau Gulam Scander Visram pichani
Mjane wa Marehemu katika picha na Mh.Nkwama wakati Ibada ya Mazishi ikiendelea
 Utapata kuona tukio zima katika Video hapa hapa BUKOBAWADAU Blog
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akitoa salam za rambirambi
 Ndugu Godwin Barongo ambae ndiye mtoto Mkubwa wa Marehemu akitoa neno la shukrani.


Sehemu ya Wanakwaya.
Ni ukweli ulio wazi kuwa hakuna Kasisi, padre, askofu, mchungaji anayeweza kutoa mahubiri pasipo kugusia Dunia na Kifo.
Waombolezaji Wakiendelea kusikiliza na kuyapokea mahubiri
Ndugu Thomas Katikilo rafiki wa Karibu wa Marehemu Kapteni Mstaafu John Barongo.
Watoto wa Marehemu wakiwa na nyuso za huzuni wakati wa ibada ya Marehemu Baba yao
Kushoto anaonekana Ndugu Novatus Nkwama
Watu mashuhuri kutoka maeneo na  mikoa wameshiriki mazishi hayo jioni ya leo Jumamosi Oct 25 kijijini Kanazi Wilaya ya Bukoba Vijijini
 Padre akiendelea kutoa mahubiri juu ya kifo.
 Watu ni wengi sana walioweza kushiriki Maziko haya
 Sehemu ya Viongozi wa Chama yupo Mh. Nkwama,Mh. Yusuph Ngaiza, Mh. Kanati Mh, Mrungi na wengineo wengi kama utavyo jionea katika mwendelezo mzima wa Matukio .
 Taswira mbalimbali Ibada Ikiendelea
 Waumini katika hali ya Utulivu na Usikivu

 Padre anaendelea kusema;Wapendwa katika Kristu, wazo kuu la masomo ya leo ni uzima wa maisha ya jayo Yaani maisha mapya baada ya kifo.
Zaidi ya nusu ya mahubiri ya kwanza yaliyohubiriwa yalikuwa kuhusu ufufuo.Kama utavyoweza kujionea katiba Video yetu iliyopo mwishoni kabisa mwa ukurasa huu.
Taswira kwa mbali wakati Ibada ya Mazishi ikiendelea


Sehemu ya Waombolezaji wakiendelea kushiriki Ibada
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Mstaafu Issa Njiku
Jeneza lenye mwili wa Marehemu Kapteni Mstaafu John Barongo.
Timu nzima ya BUKOBAWADAU BLOG tunatumia fursa hii kuwapa wapa pole wafiwa,Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!
Wananchi waliofika kushiiki Ibada ya mazishi hayo. 
 Mzee Yahaya Kajuna pichani kushoto na  Mzee Mpanju wakishiriki katika Maziko hayo
Wakuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa na Viongozi wa Chama
Sehemu ya Waombolezaji.
Mh.Wasira akiongoza zoezi la kushuhudia mwili wa Marehemu Kapt.John Barongo.
Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa mwili.
Ni muda wa kushuhudia kama anavyo onekana Ndugu Didas Zimbihile.
Ndugu Kelvin na Mzee Asiel wakati wa kushuhudia
Ndugu Divo Rugaibura aka Serikali.
 Katika hali ya  huzuni mkubwa anaonekana Mama Lugusha wakati wa zoezi la kushuhudia .
 Watu mbalimbali wakiendelea kutoa heshima za mwili kuaga mwili wa Marehemu Kapt. Mstaafu John Barongo
Simanzi na majonzi vikitawala wakati wa kuwaga mwili wa marehemu Kapt. Barongo
Muonekano wa Jeneza mara baada ya zoezi la kushuhudia
Maombi ya mwisho kabla ya kuelekea eneo la makaburi.
 Maji ya Uzima yanahusika.
Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa katibu wa CCM katika Mikoa mbalimbali,Marehemu Kapteni mstaafu John Barongo
 Umetangulia nasi tupo nyuma yako...pumzika kwa amani Mzee wetu, mshauri wetu, baba yetu kiongozi wetu Marehemu Kapteni John Barongo
Jeneza likishushwa kaburini kwa kutumia kamba
Jeneza likiwa kaburini
.. Wewe ni mavumbi na mavumbini wewe utarudi”
Hivi ndivyo ilivyo kwa mwanadamu kutokana na mapokeo ya dhehebu lake kuwa .... Sisi sote tuko upande mmoja na Biblia iko upande mwingine. ..... hivyo “miili yetu ni mavumbi na itarudi mavumbini” kutokakana na maandiko..
Pichani anaonekana Mdau Mzee Ishengoma kutoka Kemondo, pembeni yake ni Afisa Utamaduni Manispaa ya Bukoba Ndg Rugeiyamua
 Wanafamilia wakiendelea kushiiki Mazishi hapo.
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Utaribu Bw Steven Wasira akiweka Udongo.
 Sehemu ya Wanafamilia  wakiweka Udongo kumuaga Mpendwa wao.
Mama akiweka Udongo kaburini.
Zoezi la kuweka Udongo likiwa linaendelea.
Pembezoni wakati shughuli ya Mazishi ikiendelea.
Utaratibu kwa wanafamilia na Viongozi kuweka Udongo ukiendelea
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Costansia Buhiye
BUKOBAWADAU BLOG tunatoa pole kwa familia ya Mzee wetu  Kapt. Mstaafu John Barongo  tunatoa pole kwa watoto wa Marehemu ndugu jamaa na marafiki.
Watoto 8 wa Kike wa kuzaliwa na Marehemu Kapteni Mstaafu  John Barongo wakishiriki mazishi
Wafiwa  mikononi wakiwa na mashada ya maua
Shughuli ya Maziko ikiendelea
 Watu ni wengi kweli kweli...
Mh. Wasira  akiweka shada la maua katika kaburi la kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi Marehemu Kapteni Mstaafu John Barongo.
Wapili kuweka shada la Maua ni Mkuu wa Mkoa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe.
 Eng.Erasto Mashume akiweka shada la Maua katika Kaburi la Shemeji yake.
  Ndg Laurean Rugambwa Bwanakunu akiweka shahada la maua
 Baadhi ya wafiwa wakishiriki zoezi la kuweka mashada katika kaburi la Marehemu Kapt. Barongo
 Ndugu Godwin Barongo akiweka Shada ya Maua katika kaburi la marehemu Baba yake mpendwa.
 Watawa wakiweka Mishumaa katika kaburi.
Mjane wa marehemu akiweka Mshumaa katika Kaburi la mmewake mpendwa.
Mzee Abdul Kananga pichani kushoto akifuatiwa na Mzee Maulid Kambuga na Ndg Didas Zimbihile
Mh.Lwakatare akifanya kusalimiana na Mmoja wa Wazee.
WASIFU WA MAREHEMU KAPTENI (MSTAAFU) JOHN  RWEZAURA BARONGO- 1943-2014.

Kuzaliwa

Kapteni Mstaafu John Rwezaura Barongo alizaliwa na Omulangira Richard Barongo na Omwamikazi Ma Mukarukamirwa katika Kijiji cha Katoju, Wilaya ya Bukoba vijijini, Mkoa wa Kagera mwaka 1943.
ElimunaMafunzo:
Kapteni John Barongo ni muhitimu wa kidato cha nne na alipata mafunzo ya kijeshi katika chuo cha kijeshi Monduli na kupata mafunzo ya uongozi.
Capt.Barongo alipendana kuthamini sana elimu kwake na kwa wanawe na ndio maana kabla ya  kifo chake alitegemea akutunukiwa mwakahuushahada ya sheria kutoka chuokikuu huria cha Tanzania yaani LLB from Open University of Tanzania.
 Utumishiwaumma:
CaptBarongoalikuwamtumishiwaummanahasakatikachamakwatakribanimiaka 50, alianzautumishi wake katikachama cha TANU mwaka 1963 akiwa kijana mdogo sana wamiaka 20 hadi alipostaafu mwaka 2011 akiwa katibu wa Mkoa wa Chama cha Mapinduzi.
 Nafasi alizotumikia ni kama zifuatazo katika mikoa mingi ikiwemo:-
1.    Katibu mtendaji wa WilayazaSingida na Mbinga
2.    Katibuwa CCM na Mkuu wa Wilaya za Bukoba,Mpwapwa na Biharamulo. Wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba ni kipindi nchi yetu ilipokuwa kwenye vita ya Kagera ya kumuondoa Nduli Idd Amin mwaka 1979.
3.    Katibuwa CCM wa Mikoaya: Kigoma, Kagera, Mara,  Manyara, Shinyanga, Dar es salaam na Dodoma alikostaafu mwaka 2011.
Tuzo ya utumishi
Kwa kuthaminiutumishi wake wamudamrefukatika Chama cha Mapinduzi; HalmashauriKuuya Chama Cha Mapinduzi- Taifa, kupitia kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania ilimtunuku 
TUZO YA UONGOZI NA UTUMISHI ULIOTUKUKA alipostaafu Mwaka 2011.

Utumishikwenye Bodi mbalimbali:

CaptBarongoalitumikiataifakatika bodi mbalimbali nchini na muda mwingi akiwa kwenye Bodi ya chama kikuu cha ushirika mkoawa Kagera(KCU)na hivi karibuni alikuwa mjumbewa Bodiya DUWASA(Dodoma Urban Water Supply & Sewage Authority) naalikuwa pia Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Chamber Commerce, Industries and Agriculture(TCCIA) wamkoawa Dodoma.

Shughulibaadayakustaafu:

Mara baadayakustaafualikuwanimkurugenzimtendajiwakampuniyake Triangle Security Services pia akiwa na kiwanda kidogo cha kusindika mafuta ya Alizeti. Kwa sababu hiyo, alikuwa mwanachama wa chama cha wasindikaji wa mafuta ya Alizeti.
Shughulimbalimbalizakijamii:
Kwa wale wanaomfahamu, waomjuanawaliofanyakazina Capt John Barongowanasemakuwaalikuwamtuwawatukwamaanakuwaalikuwamshirikiwashughulizakijamii. Alipenda sana watu, alikuwana utu na alikuwa mkarimu. Alikuwa pia mpenzi wa michezo kwa vijana. Alikuwa mtumishi wa umma wa kweli na mwadilifu namuumini mzuri wa kanisa katoliki.
 FamiliayaBarongo:
Marehemuameachafamiliayenye mke (Ma Winfrida),watoto 10(Placidia, Consolata, Jane, Godwin, JohnMary, Benedicta, Jovita, Edwin, Johanitana Lilian- ambao wote wameo ana kuolewa.  Pia ameacha wajukuu 27 nav itukuu watatu.
Capt.Barongo alikuwa ndio mkuuwa familia ya baba yake Omulangira Richard Barongo. Kwa watoto wamarehemu wanasema baba yao alikuwa ni mcheshi, mpole, mthamini elimu, mzee mwenye misimamo lakini anashaurika, alikuwa mpenda watu namuadilifu. Alipenda mshikamano kwa familia yake, na kwa watoto aliwaasa kuwa katika hali yoyote ile wawe na umoja kwa mazuri na magumu.
Amewaachia watoto wote Elimu wakiwa ni watu wazima nawana elimu yakuwa wezesha kuishi na kujitegemea. Watoto hawa sasaw anabaki na kiongozi wa familia yao Ndugu Godwin Barongo ambaye ndie mtoto mkubwa wa kiume na ambaye tuko kwake hapa leo Pugu Kajiungeni.
Historiayaugonjwa:
Amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa shinikizo la damu na matatizo ya moyo tangu mwaka jana alikwenda kutibiwa India na aliporudia lijisiki nafuu sana.
 Baadaye matatizo yalirejea na mapema mwezi huu aliletwa katika Hospital yaTaifa ya Muhimbilikwamatibabu zaidi. Jumapili hali ikabadilika  ghafla na mapema Jumatatutarehe 20 Oktobasaa 5:30 asubuhi akaaga dunia.
Shukrani:
Familia yaCapt Barongo inapenda kutoa shukrani kwa madaktari na wauguzi wote wa Muhimbili ambao walijitahidi kuokoa maisha yake. 
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LI
HIMIDIWE!!
TAZAMA VIDEO SEHEMU YA KWANZA SALAAM ZA RC, ALICHOKISEMA MH WAZIRI WASIRA NA NENO LA FAMILIA
TEMBELEA UKURASA WETU WA FACEBOOK KWA MATUKIO YA  PICHA ZAIDI YA 200 KUPITIA LINK HII>>Bukobawadau Entertainment Media
Next Post Previous Post
Bukobawadau