Bukobawadau

KATIKA PICHA MKUTANO WA BAWACHA ULIOFANYIKA UWANJA WA UHURU MJINI BUKOBA LEO OCT 29,2014

Sehemu ya wanachi wa Manispaa ya Mji Bukoba waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara wa Viongozi wa BAWACHA uliofanyika jioni ya leo Oct 29 Katika Uwanja wa Uhuru Mjini hapa.
Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Uhuru Mjini Bukoba Mwenyekiti Bawacha Mhe. Halima Mdee amesema Chadema hawatakubali kupigia kura ya ndiyo rasimu ya  katiba inayopendekezwa kwani wananchi wakipendekeza katiba mpya  iweke wazi mikataba inagusa maslahi ya wananchi kwa kuhakikisha mikataba anayoingia rais inakuwa wazi katika magazeti ya serikali ili wananchi wajue watakavyonufaika na mikataba hiyo lakini katiba inayopendekezwa imetupilia mbali maoni hayo ambapo amesema  katika hiyo imejaa mapendekezo ya kulinda maslahi ya wachache na sio  wananchi masikini walio wengi.
Sehemu ya Viongozi  waliokaa eneo la Meza Kuu.
 Katikati ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare
Pichani kulia ni Mh.Diwani kata ya Rwamishenye Ndugu Dismas Rutagwelera
Kutoka kushoto ni naibu katibu  na mratibu wa uhamasishaji BAWACHA Bi  Kunti Yusuph, Katibu Grace Tendega,Mwenyekiti Bawacha Mhe. Halima Mdee.
 Naibu Katibu wa Bawacha Taifa Kunti Yusuph
 Umati wa watu ukiendelea kumsikiliza Naibu Katibu wa Bawacha Taifa Bi Kunti Yusuph
Akizungumza katika mkutano wa hadhara jijini Mwanza Naibu Katibu wa Bawacha Taifa Kunti Yusuph amesema kuwa wananchi hasa wanawake wanapaswa kuelewa kipaumbele chao katika maisha yao ya kila siku.

 Bi Kunti amewataka Wanawake kujua kuwa kipaumbele katika maendeleo yao ni kupata huduma bora za afya na kuepuka na mateso na manyanyaso yanayojitokeza na wala sio uwiano sawa wa asilimia hamsini kwa hamsini.
Makamu mwenyekiti bara Hawa Mwaifunga akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mjini Bukoba jioni ya leo Oct 29,2014 

 Wanahabari wakiwajibika.
Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni katibu wa mkoa, Mama Concesta Rwamlaza akiongea na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika Mkutano wa BAWACHA hii leo Mjini Bukoba
 Taswira wakati Mkutano unaendea
 Mwenyekiti Bawacha Mhe. Halima Mdee akikabidhiwa zawadi kutoka kwa Wanawake  Chadema  Kata ya Hamugembe Mjini Bukoba.
 Shukrani kutoka kwa Viongozi wa BAWAACHA mara baada ya kukabidhiwa zawadi.
 Taswira Uwanja wa uhuru Mjini Bukoba wananchi wakifuatilia tukio la zawadi kwa Viongozi wa BAWACHA
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo taifa, BAWACHA Bi. Halima Mdee.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa BAWACHA taifa Bi. Halima Mdee amesema kuwa kwa kuwa wanaamini ni rahisi kudanganyika kwa uwiano sawa katika Serikali lakini hilo halimsaidii mwanamke kuweza kupata mahitaji yake muhimu ikiwemo huduma izo za afya.
 Mdee akiendelea kuongea na wakazi wa Mji wa Bukoba amewataka wananchi wa jiji la Mwanza wasikubali kulazimishwa kuikubali katiba inayopendekezwa kwani haikuzingatia maoni ya wanachi ya kutaka uwazi katika rasilimali za nchi zilizopo zitumike kunufaisha wananchi badala yake katiba hiyo inawapa mamlaka vigogo kuendelea kunufaika na rasilmali za taifa huku wananchi wakiendelea kuumia.
Ghafla anajitokeza Kijana akiwa na Kadi ya CCM na kuikabidhi kwa Mhe. Halima Mdee
 Mara baada ya kukabidhi Kadi hiyo kwa Mwenyekiti Bawacha Mhe. Halima Mdee


Kijana huyo anapewa nafasi ya kuongea na wananchi kuhusu sababu iliyomfanya arejeshe kadi ya Chama tawala CCM
  Mwenyekiti Bawacha Mhe. Halima Mdeea akikabidhi  Kadi nyingine Mwanachama mpya.
Ishara ya kuitikia Kampeni ya BAWACHA isemayo.. 'Delete CCM, Futa Kabisa'...
Akiendelea kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Uhuru Mjini Bukoba 
 Katibu Grace Tendega akiongea kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Uhuru Mjini
 Sehemu ya Wadau wakifuatilia kinachojiri.
Mama  Concesta Rwamlaza Mbunge  Chadema viti Maalum (Bukoba)
Mwenyekiti wa Wilaya ya Bukoba mjini, Ndugu Victor Sherejeh akifunga mkutano huo uliokuwa na Agenda kuu zifuatazo :
  i) Kuwahamasiha wanawake kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura
(BVR)
ii) Kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa
iii) Kuwaelimisha na kuwa na mtazamo sahihi wa katiba mpya ijayo

 iv) Kuwahamasisha kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
v) Kubaini na kuwatia shime wagombea wanawake makini katika nafasi mbalimbali
kwenye chaguzi hizi

  Mwisho wa yaliyojiri katika Mkutano wa BAWACHA Mjini bukoba leo.
Fanya ku like ukurasa wetu wa facebook UPATE  matukio ya picha ZAIDI ya 200  kupitia hapa>>Bukobawadau Entertainment Media

Next Post Previous Post
Bukobawadau