Bukobawadau

AMSHA AMSHA NDANI YA MJINI BUKOBA DESEMBA 2014

Kama kawaida ya mwezi Desemba  Amsha amsha za hapa na pale ndani ya Manispaa Bukoba,tayari mji umechangamka kwa wingi wa heka heka na shamrashamra  mbalimbali.
 Tunakutana na wageni wanao endelea kuingia Mjini hapa  kwa ajili ya Msimu huu wa sikukuu
 Mji wa Bukoba, hapa ni barabara ya Jamhuri ..hebu check Watoto wa  Kihaya walivyo ng'ari ng'ari!!
 Mama na mwana pichani ni Bi Grace Rwihula na mwanae wa kwanza kumzaa
Wanaonekana walivyo na furaha na maisha yao,Wapo kamili ni familia ya Mr & Mrs Datus Lwihula 
 Uso kwa uso na 'Makusalo na Waya'maarufu kwa jina la Revocharth Minja
 Mr. Revocharth Minja katika picha na Wafanyakazi wenzake wa TPA
 Hali ya Usafiri  Mjini hapa ni Changamoto kubwa,ni dhahiri mabasi yanatumika mengine ni mabovu  ,Camera yetu inashuhudia (sehemu yenye duara pichani) Abiria wakipata taharuki baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupasuka sehemu ya bodi kutokana na Wingi wa watu
 Basi la Bunda lenye Nambari T805 BDW linalotokea Karagwe kwenda Mwanza ,pichani likiingia  ndani ya Stendi Kuu Mjini Bukoba .
  Kwa taarifa ni kwamba hali ya Usafiri ni Sheedah na hivi Meli ya MV Victoria ni mbovu ,mbovu mbovu  tena sana, Meli hiyo Ilipokuwa nzima siku za nyuma nyuma, ilikuwa inatoka Mwanza inafika Bukoba saa 12 asubuhi au ikitoka Bukoba saa 4 usiku inafika Mwanza saa 12 asubuhi,kwa sasa inafika saa 6 mchana, saa saba, saa nane, hakika ni sana 'Wakuu wetu jamani mnasubiri iuwe watu ndiyo tupate meli mpya?
 Meli ya MV Victoria inayofanya safari zake kutoka mkoani kagera kuelekea jijini mwanza juzi kati imezuiliwa kuondoka mjini bukoba kutokana ubovu ilionao hali ambayo imewalazimu wananchi waliokuwa wanataka kusafiri na meli hiyo kuandamana hadi kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa kagera  kwaajili ya kutoa malalamiko yao.
 Wakiongea nnje ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa kagera  John Mongela wananchi hao wamelalamikia kuto kuwepo kwa usafiri wa meli kwa zaidi ya mwezi moja  sasa nakwamba jana meli hiyo imewasili mjini bukoba na kuambiwa wapakie mizigo yao ndani ya meli hiyo kwaajili ya kuisafirisha  kutoka mkoani kagera kueelekea jijini mwanza ambapo wamesema wamepakia mizigo yao ndani ya meli hiyo na leo wameambiwa meli hiyo haitosafiri kutokana na meli hiyo kuwa na hitilafu taangu muda mrefu na kwamba mazao yao biashara sasa  yamekuwa yakiharibika ndani ya meli hiyohali mabayo imewalazimu wananchi hao kuandamana mpaka kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa kagera kwaajili ya kutoa malalamiko yao  juu ya meli hiyo.
 Akizungumza na wananchi hao mkuu wa wilaya ya bukoba Bi.Sipora Pangani amewataka wananchi  hao kuwa na subira  nakuwataka waondoke katika ofisi hizo  huku akisema kuwa serikali italishughulikia suaala hilo  huku mbunge wa viti maalu Conchesta Lwamulaza akiitaka serikali kuiondoa meli hiyo kwakuwa imekuwa  ikileta hofu kubwa kwa wananchi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
 Mitaa ya Kati wadau mbalimbali wakibadilishana mawazo
 Yupo Mzee Cathbert Basibila, Mr Rahym Kabyemela na Uncle Tom maarufu kama 'Katikilo' aka Mtani jembe.
 Kama kawaida nje ya Soko kuu Senene wapo wapo kiasi.
 Mjini Bukoba ni msimu wa  kuvuna zao la senene
Ndani ya Soko kuu Mjini Bukoba.
 Kazi na Dawa, hii imekaa vizuri
 Hekaheka za hapa na pale ndani ya Soko kuu Mjini Bukoba
 Mzigo wa Vitunguu Kutoka shambani ukiingizwa Sokoni
 Kulia anaonekana Ndg Masudi katika kuwajibika
 Wanamawa wajasiliamali kama walivyokutwa na Camera yetu
 Ni Sehemu ya kwanza 'Amsha amsha'  Desemba Mjini Bukoba
 Mdau Mwarabu wa Soko kuu Mjini hapa.
 Soko la ndizi linavyo onekana
Taswira maeneo mbalimbali ndani ya Soko kuu Mjini Bukoba.
Wajasiliamali wa Soko la kuu Mjini Bukoba katika biashara zao.
Amsha amsha fukweni Kiroyera,Siku moja kabla ya tamasha la Bukoba Carnival lililofanya Jana jumamosi na kufana ile mbayaaa!
 Boti maalum kutoka kampuni ya WALKGARD & TOURS
 Kijana mpambanaji Erasmus George 'Kempe' na Mr.James  Njuu.
 Katika maandalizi ya Tamasha la Bukoba Carnival ambayo matukio yatakufikia badae leo.
Fukweni Kiroyera 
 Mrs Willy Kiroyera Rutta
 MUHIMU :BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
Katika hili na lile Kijana Ras na Mr Willy Kiroyera Rutta

Next Post Previous Post
Bukobawadau