Bukobawadau

MKURUGENZI AMTIMUA MWANDISHI WA HABARI

Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ngara Ndg. Cornel Ngudungi  (mwenye miwani) akiwa katika moja ya mikutano yake.
 Mwanahabari wa Radio na magazeti Mkoani Kagera Shaaban Ndyamukama  katika kuwajibika 
NGARA.
Wakati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya  Kikwete akisisitiza watendaji wa serikali  kufanya kazi na vyombo vya habari hali imekuwa tofauti kwa baadhi yao na kulazimika kuwatimua wanahabari kwenye ofisi zao
Hali hiyo imejitokeza jana wilayani Ngara  mkoani Kagera ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri  ya wilaya hiyo Cornel Ngudungi  alipomfukuza mwandishi wa habari  Shaaban Ndyamukama aliyetaka kujua maendeleo ya kampeni za uchaguzi
Ngundungi ametoa kauli hiyo  ofisini kwake  muda mfupi baada ya kumfukuza mwandishi huyo  kwa madai kuwa anaandika  habari  za  kuichafua  halmashauri  ya wilaya hiyo na kukiuka maadili ya uandishi
Mkurugenzi huyo amesema  haoni umuhimu wa kutumia vyombo  vya habari kutoa taarifa za maendeleo  kwa wananchi kwa madai kuwa  yeye hataki kuandikwa wala kutangazwa kwenye vyombo vya habari
Ngudungi amesema  haoni haja  ya kufanya kazi na vyombo vya habari kwa sababu baadhi ya  waandishi wanapotosha jamii kwa kuripoti taarifa zisizo sahihi hali ambayo  inapelekea  kulaumiwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa
“Nilitumwa kufanya kazi za wananchi sio na waandishi wa habari wananchi wakishaona ninawafanyia nini inatosha” aliongeza mwandishi anayepewa habari na kuiandika kinyume na jinsi alivyopewa siwezi kushirikiana naye” Alisema
Akizungumza na wanahabari wenzake nje ya ofisi ya mkurugenzi huyo mwandishi huyo amesema alifika kutaka kujua idadi ya vituo vitakavyoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa wilayani humo na jinsi kampeni zilivyo na changamoto zake
 Ndyamukama amesema kwa kuzingatia na kufuata misingi ya Katiba, sheria, kanuni na taratibu  wananchi wanayo haki ya kupata habari kupitia chombo chochote cha habari kama vile Radio Magazeti na Luninga
Imedaiwa kuwa mwanahabari huyo aliandika taarifa za mmoja wa wafanyakazi kazi wa kituo cha Afya cha Lukole aliyetuhumiwa kuwapiga  wagonjwa na kwamba taarifa hizo zilikuwa bado kuhakikiwa na mkurugenzi huyo
Hata hivyo mkuu wa mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu amelaani kitendo hicho cha mwanahabari kufukuzwa akitafuta taariza za maendeleo ya wananchi na kudai kuwa atafuatilia kujiridhisha ili hatua zichukuliwe
“Kama hali hiyo imejitokeza badi mkurugenzi anahitaji kuelimishwa kwani wananchi wana haki ya kupewa taarifa za maendeleo ya halmashauri na masuala mengfineyo kwenye wilaya yao” Alisema Kanyasu
Pamoja na hayo imefahamika kuwa baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wakiwemo wakuu wa idara hawana mamlaka ya kutoa taarifa za maendeleo kwenye vitengo vyao na kusababisha baadhi yao kulalamikiwa na wananchi.
Wilaya  ya Ngara inavyo vijiji 75 vyenye  vitongoji 394 vitakavyotumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa  na idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ni 133,317  sawa na 134%  kati ya  walengwa  99, 259  kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 .
Next Post Previous Post
Bukobawadau