CRISTIANO RONALDO NDIYE MCHEZAJI BORA WA FIFA DUNIANI MWAKA 2014
Tuzo ya mchezaji Bora wa dunia wa Fifa kwa mwaka 2014 tayari
imetangazwa hivi punde ambapo Mshambulia wa Real Madrid na timu ya
taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ndiye mshindi wa tuzo hiyo
inayojulikana kwa jina la FIFA Ballon d'Or 2014.
Ronaldo kawapiga
chini wachezaji wenzake wawili walikuwa wamebaki kwenye fainali ambao
Lionel Messi mshambuliaji wa Barcelona na mchezaji wa timu ya taifa ya
Argentina na Manuel Neuer Mlinda mlango wa Bayern Munich ambaye pia
hudakia timu yake ya taifa ya Ujerumani.
Katika hisia kali anaonekana Ronaldo mara baada ya kuwapiga chini Lionel Messi na Manuel Neuer
Rais wa FIFA Sepp Blatter pichani (kulia) akimpongeza Ronaldo baada yakushinda tuzo ya mchezaji bora kwa mwaka 2014.
Cristiano Ronaldo baada ya kutwaa tajila mwaka 2014 ikiwa ni baada ya miezi 12
Cristiano Ronaldo ( kushoto) katika picha ya pamoja na Mshindi wa tuzo ya FIFA kwa Wanawake Nadine Kessler kwa mwaka 2014
Mchezaji Cristiano Ronaldo (kulia) akiurahi na na mtoto wake Cristiano Jr mara baada ya kushinda Tuzo ya mchezaji Bora wa dunia wa Fifa kwa mwaka 2014( FIFA Ballon d'Or 2014)
Ronaldo anafurahia ukodak na Ma Msapu, Bi Marta kabla ya kutangazwa kwa tuzo ya mshindi wa FIFA muda mchache uliopita usiku huu wa Jumatatu Jan 12,2014
Ronaldo muda mchache kabla ya kushinda tuzo hii ya tatu kwake na ya pili kwa mfululizo mfululizo 2013/2014 ,tumpe hongera zake
Muonekano wa Mchezaji Messi (kulia) na mpenzi wake Antonella Roccuzzo katika ( Red Karpet)
Katika picha ni sehemu ya wachezaji walio chaguliwa katika timu ya dunia ya FIFA