Bukobawadau

MABADILIKO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI

Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo asubuhi, Rais Jakaya Kikwete ametangaza marekebisho ya Baraza lake la Mawaziri.

Taarifa iliyotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue leo, imesema, nafasi iliyoachwa na Profesa Muhongo sasa itashikwa na George Simbachewene, huku nafasi ya Waziri wa Nhi Ofisi ya Rais, Oratibu na Bunge ikichukuliwa na Dk. Mary Nagu.

Kulingana na taarifa hiyo, aliyekuwa Waziri wa Chakula na Kilimo Christopher Chiza anakuwa Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji, huku Dk. Harisson Mwakyembe akipewa nafasi ya Uwaziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Waziri William Lukuvi anakuwa waziri wa Ardhi na Nyumba ya Makazi nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Profesa Anna Tibaijuka kabla ya kujiuzulu kufuatia sakata la Tegeta Escrow Account.

Naye Stephen Wasira katika mabadiliko hayo, anakuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, wakati aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta anakuwa Waziri wa Uchukuzi huku Jenista Mhagama akipewa nafasi ya Uwaziri wa Sera na Uratibu wa Bunge.

Taarifa imesema, aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba Kairuki anakuwa Naibu wa Ardhi Nyumba na Makazi, huku Steven Masele akipata nafasi ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano.

Wengine ni Anna Kilango anayekuwa Naibu Waziri wa Elimu, Ummy Mwalimu Naibu wa Sheria na Katiba na Mwijage Naibu Waziri wa Nishati na Madini.
MABADILIKO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo asubuhi, Rais Jakaya Kikwete ametangaza marekebisho ya Baraza lake la Mawaziri. Taarifa iliyotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue leo, imesema, nafasi iliyoachwa na Profesa Muhongo sasa itashikwa na George Simbachewene, huku nafasi ya Waziri wa Nhi Ofisi ya Rais, Oratibu na Bunge ikichukuliwa na Dk. Mary Nagu. Kulingana na taarifa hiyo, aliyekuwa Waziri wa Chakula na Kilimo Christopher Chiza anakuwa Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji, huku Dk. Harisson Mwakyembe akipewa nafasi ya Uwaziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Waziri William Lukuvi anakuwa waziri wa Ardhi na Nyumba ya Makazi nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Profesa Anna Tibaijuka kabla ya kujiuzulu kufuatia sakata la Tegeta Escrow Account. Naye Stephen Wasira katika mabadiliko hayo, anakuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, wakati aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta anakuwa Waziri wa Uchukuzi huku Jenista Mhagama akipewa nafasi ya Uwaziri wa Sera na Uratibu wa Bunge. Taarifa imesema, aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba Kairuki anakuwa Naibu wa Ardhi Nyumba na Makazi, huku Steven Masele akipata nafasi ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano. Wengine ni Anna Kilango anayekuwa Naibu Waziri wa Elimu, Ummy Mwalimu Naibu wa Sheria na Katiba na Mwijage Naibu Waziri wa Nishati na Madini.
Next Post Previous Post
Bukobawadau