Bukobawadau

PROF.IBRAHIM LIPUMBA APANDISHWA KIZIMBANI

Mwenyekiti wa CUF amepandikishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amepandikishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu
Jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shtaka moja ya kuwashawishi wafuasi wa chama chake kufanya kosa la jinai.
Awali kabla ya kufikishwa katika mahakama hiyo Profesa Lipumba alifika katika kituo cha polisi ambapo alitakuwa kuripoti yeye na viongozi wengine wa chama hicho ambao walikamatwa katika tukio la maandamano na badaa ya kiongozi huyo kuzungumza na polisi aliruhusiwa kuondoka na ndipo alipozungumza na waandishi wa habari kulaani kilichofanywa na polisi.

Akisimulia namna alivyopata kipigo hadi kupasuka sehemu ya kichwani naibu mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho Bw Abdul Kambaya amesema anakumbuka silaha mbalimbali zilitumika ikiwemo spana na kufungua tairi ya gari ambayo ndio iliyomjeruhi kichwani
   Wakati viongozi hao wa CUF wakiendelea kufanya mahojiani mbalimbali na waandishi wa habari alikuja afisa mmoja wa polisi na kumwita profesa Lipumba na kuondoka naye kuelekea katika moja ya ofisi zilizopo kituoni hapo ambapo baada ya muda wa takribani saa moja na nusi hali ya kiongozi huyo ilibadilika na kukimbizwa katika kituo cha afya cha umoja wa mataifa kilichopo karibu na viwanja vya Leaders akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshia polisi katika gari lenye namba za usajili Pt 2566 aina ya rav 4.

Baada ya matibabu msafara wa polisi ulielekea katika mahakama ya kisutu ambapo wakili wa serikali Joseph Maugo mbele ya hakimu mkazi Mh Isaya Arufani aliiambia mahakama kuwa kati ya tarehe 22 na 27 jan mwaka huu akiwa kama kiongozi wa chama aliwashawishi wafuasi wake kutenda kosa la jinai na kuongeza kuwa upelelezi haujakamilika na hawana pingamizi na dhamana.

Upande wanasheria wanaomtetea Mh Lipumba wapo sita wakiongozwa na wakili Mohamedi Tibanyendela na Peter Kibatala ambapo
Waliomba mahakama itoe masharti mepesi ambapo Mh Lipumba yupo nje kwa dhamana ya watu wawili waliosaini bondi ya shilingi milioni mbili na shauri hilo litatajwa tena Feb 26 mwaka huu
Next Post Previous Post
Bukobawadau