Bukobawadau

Sugu anusurika kifo, apata ajali mlima Kitonga

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' amenusu kifo baada ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali katika eneo la mlima Kitonga mkoani Iringa.
Taarifa za awali kutoka kwa katibu wake Kwame Anangisye zimeeleza kuwa Mbunge huyo akiwa na watu wanne kwenye gari yake alipata ajali hiyo mwanzoni mwa mlima Kitonga akitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.
 “Tulipoanza kushuka kwenye mlima Kitonga gari ya Mbunge ilifeli breki na kisha kupinduka mara moja na kugeukia ilikotokea, ilikuwa ajali mbaya lakini tunashukuru Mungu  tumepona.
Amesema pamoja na ajali hiyo kuonekana  mbaya kwao,  wanamshukuru Mungu kwani waliweza kutoka wakiwa salama na hakuna hata mmoja aliyepata maumivu makali.
Next Post Previous Post
Bukobawadau