Bukobawadau

Uandikishaji Vitambulisho vya kura vipya kuanza Februari.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini, mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo, mjini Dodoma.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika mkutano wa Baraza hilo leo, mjini Dodoma.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakisoma nyaraka za  mkutano wa Baraza hilo leo, mjini Dodoma.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakisoma nyaraka za  mkutano wa Baraza hilo leo, mjini Dodoma.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (walio kaa mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa  Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kufungua  Mkutano huo, leo, mjini Dodoma.

 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Na. Mwandishi Maalum


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka amesema kuwa Serikali inatarajia  mwezi Februari mwaka huu kuanza  uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura  kwa kutumia teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR) ili kuboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura ambapo maboresho hayo yatafuta matumizi ya vitambulisho vya kupigia kura vya sasa.


Turuka alifafanua kuwa maboresho ya daftari hilo nchini yatafanyika kwa watu wote wenye sifa za kupiga kura Oktoba mwaka huu na kukamilika kabla ya kura ya maoni ya Katiba,  katika kura ya maoni ya Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu wa 2015, mpigakura atatumia kitambulisho kipya atakachopatiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), baada ya kuandikishwa upya katika mfumo huo.



Akiongea mara baada ya kufungua Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo, mjini Dodoma, Turuka alibainisha kuwa tayari  serikali imefanikiwa kuifanyia majaribio teknolojia hiyo ya BVR katika majimbo matatu ya hapa nchini ambayo ni; Jimbo la Kawe – Dar es Salaam ,  Jimbo la Kilombero - Morogoro na Mlele - .

“Serikali imefanikiwa kutekeleza kwa ufanisi  jaribio la teknolojia ya BVR japo ambapo  changamoto zilizo jitokeza katika majaribio hayo tayario tumeshazifanyia kazi katika kuboesha zoezi hilo, hivyo napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa teknolojia hiyo ya kisasa kuwa lengo la serikali la kutumia teknolojia hiyo ni kumuwezesha mwananchi kujiandikisha kupiga kura kwa kutumia njia ya kisasa hivyo nawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi wakati zoezi hilo litakapo anza  kwani tunaandikisha wapigakura   ” alisistiza Turuka

BVR ni mfumo wa kuchukua taarifa za mtu za kibaiolojia hasa alama za vidolya e kwa ajili ya kuzihifadhi katika kanzidata (database) kwa ajili ya utambuzi. Mwaka 2004, NEC ilianzisha Daftari la Kudumu la Wapigakura ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa taarifa za wapigakura na uhifadhi wa taarifa za kielektroniki. Wapiga kura wa zamani kwa maana waliokuwa kwenye daftari la sasa watatakiwa kwenda katika vituo vya kujiandikisha kuchukuliwa taarifa zao hasa za vidole, picha na saini zao katika mfumo mpya wa BVR na hatimaye kupewa vitambulisho vipya .

Mwisho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau