Bukobawadau

MBOWE:TUTAAKIKISHA KILA MWANANCHI AMEJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA LAKINI KWA UPANDE WA KATIBA MSIMAMO WETU KAMA UKAWA UKO PALE PALE WA KUTOSHIRIKI

Viongozi wa chadema  akiwemo mwenyekiti wakiwa wanasali kwanza kabla ya mkutano wa viongozi wakanda ya kaskazini kuanza
 Naibu katibu mkuu wa Chadema Salum Mwalimu akiwa anaongea nawaandishi wahabari
 MWENYEKITI wa chama cha demokrasi na maendeleo Chadema Freeman Mbowe amesema kuwa  chama chao kimejipanga kuahakikisha kinahamasisha  kwa  nguvu zote wananchi weweze kwenda kujiandikisha katika  daftari la mpiga kura 

Alisemakuwa hii itaweza kumsaidia kila mwananchi  kuweza kupata haki yakumchagua kiongozi bora  anaemtaka  katika uchaguzi mkuu  ujao  wa kuwachagua viongozi wakuu ambao ni rais ,wabunge na madiwani.
Alisema kuwa pamoja ya kuwa tume wamekuwa wananchelewesha kufanyika kwa zoezi hili , wao wamejipanga kikamilifu na pindi ambapo zoezi hili litatangazwa  kuanza rasmi watajitaidi kwa njia yoyote kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha
Alisema kuwa kwa upande wa kupiga kura katiba wanaendelea na msimamo wao ambao walitangaza awali wa kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni ya katiba  huku akisisitiza kuwa swala la kutoshiriki katika mchakato wakura za maoni auingiliani kabisa na  kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura 

Alimaliizia kwa kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi  sana pindi pale ambapo watasikia zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu limewadia  ili waweze kupata haki yao ambayo itawaruhusu kuchgua kiongozi wanao wataka.
 

Next Post Previous Post
Bukobawadau