Bukobawadau

BUNGE LAPITISHA MUSWAADA WA SHERIA YA BAJETI YA MWAKA 2014

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha muswada wa sheria ya bajeti wa mwaka 2014 ambao unatajwa kuwa utakuwa suluhu ya kudumu ya matumizi ya fedha za umma kwa nidhamu na kuliepusha taifa na vitendo vya ubadhirifu vilivyoshamiri hapa nchini.
Akijibu hoja za wabunge mbalimbali kabla ya muswada huo kupitishwa waziri wa fedha Mhe.Sada Mkuya amesema muswada huo utawabana pia baadhi ya viongozi wa wizara wakiwemo mawaziri ambao wamekuwa na tabia ya kushinikiza taasisi ambazo zipo chini ya wizara zao kuwapa fedha za kuendesha wizara pindi bajeti ya wizara husika inapoisha kabla ya wakati.
 
Naye Mbunge wa Jimbo la Pangani Salehe Pamba pamoja na yule wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wameitahadharisha Serikali kuangalia pia utendaji kazi wa wafanyakazi wake sambamba na kudhibiti vitendo vya rushwa ili kufanya muswada huo uweze kutimiza malengo yake.
 
Kwa upande wake Mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde amesema Muswada huo utalisaidia kikamilifu Taifa la Tanzania kama pia utawasilishwa pia katika baraza la wawakilishi ili kufanya pande zote mbili za Muungano kunufaika nao.
Next Post Previous Post
Bukobawadau