Bukobawadau

Imetosha Movement Kufanya Matembezi Hisani Machi 28

Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam. Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taasisi ya 'Imetosha Movement' na viongozi wakizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni. Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taasisi ya 'Imetosha Movement' na viongozi wakizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni.[/caption] Na Mwandishi Wetu ASASI ya Harakati za Imetosha ilioanzishwa kupinga mauaji na vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye u-albino inatarajiwa kufanya matembezi makubwa ya hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kwa uma juu ya imani potofu zinazoendelea za mauaji ya albino. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu amesema matembezi ya hisani kuchangia fedha zitakazowezesha kutolewa kwa elimu kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa juu ya imani potofu zinazoendelea na mauaji ya albino yanatarajia kufanyika Dar es Salaam Machi 28, 2015. Alisema matembezi hayo yataanzia katika Viwanja vya Leaders na kuzunguka maeneo yaliyopangwa kisha kurejea viwanjani hapo kwa ajili ya shughuli maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya harakati maalumu za imetosha zitakazo kwenda kwa jamii ya kawaida na kueneza elimu ikiwa ni juhudi za kuhamasisha kila mwana jamii kupaza sauti na kusema 'Imetosha Mauaji ya Albino'. "...Baada ya taratibu kukamilika, matembezi sasa yatafanyika Tarehe 28 Machi kuanzia saa 12 Alfajiri, kutoka Leaders Club tutazunguka na kurudi hapo, karibuni sana tuchangie harakati hizi zenye lengo zuri kwa mustakabali wa Taifa letu lenye sifa ya amani na utulivu," alisema Mdimu katika taarifa yake. Aidha akizungumzia uvumi ulioenea hasa katika nchi za nje, unaodai kwamba serikali imekataza watu wenye ulemavu wa ngozi kuandaa matembezi au maandamano alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kuongeza kuwa kuna taratibu za kufuata kabla ya uandaliwa shughuli hizo. "...Hili suala sio kweli, ili ufanye mambo kama haya ni lazima upitie taratibu za kisheria ili upate kibali. Hii ni nchi na ina taratibu zake kwa hiyo tulipaswa kuzifuata na ndio kilichosababisha hata matembezi yetu kuahirishwa. "Tulikuwa tunafuata taratibu na leo rasmi tumepata usajili wa Imetosha...sasa imetosha imekuwa taasisi kamili inayoitwa IMETOSHA MOVEMENT. Napenda kuchukua wasaa huu kuwashukuru marafiki wote wanaoniunga mkono, na kunipa moyo, msinichoke kwa sababu safari bado ni ndefu," Hata hivyo aliwataka wananchi na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni kujitokeza katika matembezi hayo ya hisani ili kuunga mkono juhudi sa mapambano ya kukomesha mauaji na vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa watu wenye ualbino maeneo mbalimbali ya nchi. _________________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau