Bukobawadau

PROF TIBAIJUKA ADHAMINI MAFUNZO YA WAENDESHA PIKIPIKI WILAYANI MULEBA

Waendesha pikipiki maarufu bodaboda kutoka jimbo la Muleba kusini wakiwa kwenye mafunzo ya sheria za usalama barabarani chini ya ufadhili wa Mbunge wa Jimbo hilo Profesa Anna Tibaijuka na kuendeshwa na Chuo cha udereva cha Lake zone Driving School mkoani kagera na kikosi cha usalama barabarani mkoani humo.
Mkuu wa wilaya ya Muleba Francis Isaka amewataka vijana hao kuhakikisha wanazijua sheria na kuepuka ajali zinazogharimu maisha ya watu na wengine kuwa walemavu wa kudumu na kupungua nguvu kazi ya Taifa.
Aidha Mkurugenzi wa Lae zone Driving School mkoani Kagera Winstoni Kabantega amewaasa vijana hao kuhakikisha wanaendesha vyombo vya moto wakiwa na leseni zenye majina m halali  huku wakijihadhari na ulevi mwendo kasi na kubeba abiria zaidi ya wa chombo husika
Jumla ya vijana 411 wamejitokeza kupata mafunzo hayo ya siku nne ambapo wengie 179 waliofika kwa kuchelewa imeelezwa na mbunge Profesa Tibaijuka kwamba watapewa awamu nyingine baada ya kikao cha bajeti kukamilika mwezi june mwaka huu mkoani Dodoma
Mkurugenzi wa Lake zone Driving School mkoani Kagera Winstoni Kabantega akiongea jambo.
Kupitia Bukobawadau waendesha pikipiki hao wametoa shukrani za dhati kwa Mbunge wao Mama Anna Tibaijuka kwa kudhamini mafunzo hayo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau